Header Ads

ad

Breaking News

YANGA YANG’ANG’ANIA KILELENI, YAICHAPA TANZANIA PRISONS 2-1


Na Mwandishi Wetu, Mbeya

MIAMBA wa soka NCHIMBI, Yanga SC, wamendelea kuwa ving’ang’anizi pale kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara, baada ya leo Februari 12, 2024 kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi wenyeji wao Tanzania Prisons.


Yanga walikuwa na sherehe za miaka 89 tangu kuanzishwa kwake, hivyo ushindi huo ulipeleka furaha kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.


Kazi nzuri ya Pacome Zouzoua ilimpa nafasi mshambuliaji mzawa, Clement  Mzize kuifungia Yanga bao la kwanza dakika ya nane.


Bao la pili la mabingwa watetezi wa ligi hiyo dakika ya 45, akimalizia pasi ya beki wa kulia Kouassi Attohoula Yao.


Dakika ya 58, kipa wa Yanga, Metacha Mnata alitolewa kwa kadi nyekundu baada ya kumchezea vibaya mshambuliaji wa Tanzania Prisons nje kidogo ya boksi.


Yanga wakimtoa Farid Mussa na nafasi yake ikachukuliwa na kipa Abdultwalib Mshery.


Mpira wa adhabu uliopigwa na Jeremiah Juma Mgunda ulizama kambani dakika ya 64.


Kiungo  wa Tanzania Prisons, Zabona Khamis Mayombya alitolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 86 baada ya kuoneshwa kadi ya pili ya njano akidaiwa kujiangusha wakati akidhibitiwa na nahodha wa Yanga, Bakari Mwamnyeto.


Yanga SC inaendelea kupigwa na baridi kileleni wakiwa na pointi 40 kwa  kucheza michezo 15, ikifuatiwa na Azam FC yenye pointi 32 za mechi 14 na Simba SC pointi 30 za mechi 14.









No comments