Header Ads

ad

Breaking News

Wakazi Kilangalanga waiomba Serikali kuhamisha vyoo

Na Omary Mngindo, Mlandizi

WAKAZI wa Kitongoji cha Kilangalanga Kata ya Kilangalanga Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha Mkoa wa Pwani, wameiomba Serikali kuhamisha vyoo vilivyojengwa na vinavyoendelea kijengwa katika makazi yao.

Aidha, wameiomba kutumwa kwa wakaguzi kushuhudia vyoo vilivyopo na vinavyojengwa kwenye eneo hilo ambalo kimsingi vinahatarisha afya zao.

Wakizungumza na waandishi wa habari katika eneo hilo la Kilangalanga, wakazi Ramadhani Mkopi, Mohamed Dakawa, Fatuma Amiri, Samwel Hiza na Mjumbe Said Seleman walisema kuwa eneo hilo si sahihi.

"Waandishi wa habari, hii hapa ni njia kuu ya maji, angalia mikorosho ilivyochimbuka mpaka mizizi yote ipo nje, cha kushangaza wamejenga vyoo hivyo, wakaona haitoshi wanajenga vingine mbele ya makazi ya watu," alisema Mkopi.

Naye, Dakawa aliitaka Serikali inapotoa tenda za miradi iangalie watu wenye sifa na taaluma na si kumpa kila mtu, na kuongeza kwamba vyoo vilivyojengwa awali vilianza kuwa kero kwa harufu.

"Ipo siku nitapata pesa nitanunua matofali nitajenga ukuta utakaozuia maji yanayopita hapa, ili yakae ndani ya eneo la shule, nisimuone mtu kuja kutoboa ili maji hayo yaje kwangu," alisema Dakawa.

Fatuma na Hiza nao walizungumzia ujenzi huo waliouelezea haukufuata utaratibu wa kiafya, kwani vyoo vya awali vimekuwaa adha kubwa, huku wakihoji vyoo vinavyoendelea kujengwa.

Akizungumzia adha hiyo, Mjumbe wa eneo hilo, Seleman alisema mradi wa ujenzi wa vyoo hivyo hawakuwashirikisha wananchi, kwani wasingekubali kujengwa eneo hilo.

"Changamoto iliyopo ni utekekezaji wa miradi inayokuja hapa mtaani, wananchi hawashirikishwi, hii miradi ya vyoo kama wananchi wangeshirikishwa ni wazi wasingeikubali," alisema mjumbe huyo.

No comments