Header Ads

ad

Breaking News

SERIKALI IMEBORESHA MAZINGIRA YA UWEKEZAJI-DKT.TAUSI

Dkt.Tausi Kida, Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji akimkabidhi zawadi ya kinyago  Bi.Joy Basu, Makamu msaidizi wa shughuli za Serikali ya Marekani, Ofisi ya Ustawi wa Biashara Afrika.


Na Mwandishi Wetu

KATIBU Mkuu Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji Dkt. Tausi Kida, amasema serikali inaendelea kufanya maboresho makubwa ya Kisera na Kisheria ili kujenga mazingira mazuri ya kuvutia uwekezaji nchini. 

Dkt. Kida, amesema hayo leo Februari 26, jijini Dar es Salaam alipofanya kikao na Bi. Joy Basu, Makamu Msaidizi wa Shughuli za Serikali ya Marekani, Ofisi ya Ustawi wa Biashara Afrika, kwa niaba ya Mhe. Prof. Kitila Mkumbo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji. 

“Tunafanya maboresho ya kisera na sheria zetu, na tunatunga mpya nyingine ili kuondoa vikwazo kwa wawekezaji” alisema Dkt. Kida.

Maboresho hayo, yanakwenda sambamba na kuhamisha mfumo wa analojia ambao awali ulimtaka mwekezaji kutembelea taasisi zaidi 10 ili kukamilisha taratibu za kuwekeza nchini.

“Tumetengeneza mfumo wa kidigitali wa Dirisha la Mahali Pamoja (TeIW), mfumo huo unajumuisha taasisi saba (7) na tunafanyia kazi taasisi nyingine tano(5), ili kumwezesha mwekezaji kukamilisha.


No comments