RAIS SAMIA ASHIRIKI UZINDUZI SANAMU YA HAYATI JULIUS NYERERE ADDIS ABABA ETHIOPIA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Rais wa Kenya Mhe. William Ruto, Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na viongozi mbalimbali wakati wakielekea kwenye hafla ya uzinduzi wa Sanamu ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere iliyopo katika Makao Makuu ya Umoja wa Afrika (AU), Addis Ababa nchini Ethiopia, Februari 18, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi wa Sanamu ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere katika Makao Makuu ya Umoja wa Afrika (AU), Addis Ababa nchini Ethiopia, Februari 18, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa ameshika utepe pamoja na viongozi mbalimbali wakati Rais wa Zambia Hakainde Hichilema akikata utepe huo kuashiria uzinduzi wa Sanamu ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere katika Makao Makuu ya Umoja wa Afrika (AU), Addis Ababa nchini Ethiopia, Februari 18, 2024.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa pamoja na viongozi mbalimbali katika uzinduzi wa Sanamu ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwenye Makao Makuu ya Umoja wa Afrika (AU), Addis Ababa nchini Ethiopia, Februari 18, 2024.
Taswira ya Sanamu ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere iliyowekwa kwenye Makao Makuu ya Umoja wa Afrika (AU), Addis Ababa kwa ajili ya kutambua mchango wake katika masuala ya ukombozi Barani Afrika tarehe 18 Februari, 2024. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipiga makofi mara baada ya uzinduzi wa Sanamu ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwenye Makao Makuu ya Umoja wa Afrika (AU), Addis Ababa nchini Ethiopia, Februari 18, 2024.
No comments