Header Ads

ad

Breaking News

RAIS DKT.MWINYI AKUTANA NA UONGOZI WA CRDB

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela,wakiwa wameshika mfuko wenye nembo ya CRDB

Na Mwandishi Wetu, Zanzibar

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi amekutana na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela  na ujumbe wake Ikulu Zanzibar, Februari 20,2024.

Rais Dkt.Mwinyi amesema Serikali itadumisha ushirikiano na mahusiano na benki ya CRDB.

Mkutano huo pia umehudhuriwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango Zanzibar, Mhe. Dkt. Saada Mkuya Salum na wakurugenzi mbalimbali wa Serikali kutoka Wakala wa Serikali Mtandao Zanzibar, Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Zanzibar na Taasisi ya Afisi ya Rais Ufuatiliaji na Usimamizi wa Utendaji Serikalini.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akizunvgumza na watendaji wakuu wa Benki ya CRDB


Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela akizungumza katika kikoa kilichofanyika Ikulu Zanzibar




No comments