Header Ads

ad

Breaking News

NHIF YATAKIWA KUTOA ELIMU ZAIDI KWA JAMII KUJIUNGA NA BIMA YA AFYA

 


Na WAF – Dodoma

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Afya na Maswala ya UKIMWI imetaka Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) kuongeza ufanisi, ubunifu wa kutoa elimu juu ya wananchi kujiunga na bima ya afya ili kuwa na wanachama wengi watakaochanga na mfuko kuweza kuwa endelevu.

Rai hiyo imetolewa leo Jijini Dodoma na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Afya na Maswala ya UKIMWI, Mhe. Stansilaus Nyongo baada ya kupokea taarifa ya hali ya utendaji na majukumu ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya.

Mhe. Nyongo amesema kuna haja kubwa ya kusogeza elimu kwa wananchi waliopo katika ngazi ya msingi ili kuwa na uelewa na umuhimu wa bima ya afya kabla ya kuanza kutekeleza sheria ya bima ya afya kwa wote.

“Nina imani kubwa mkifanikiwa katika kutoa elimu kwa jamii ya ngazi ya msingi sheria ya bima ya afya kwa wote ikianza kutekelezwa wananchi watakuwa tayari wana uelewa juu ya kuwa na bima ya afya,” amesisitiza Mhe. Nyongo.

Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Dkt. Faustine Ndugulile ametoa wito kwa uongozi wa NHIF pamoja na Wizara ya Afya kufanya tafiti mbalimbali juu ya uendeshaji wa mfuko wa Taifa wa bima ya afya ili kupata ujuzi namna ya kuendesha mfuko huo wakati sheria ya bima ya afya kwa wote itakapo anza kutumika.

Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu, akizungumza kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Afya na Masuala ya UKIMWI

        

No comments