Header Ads

ad

Breaking News

MSAFARA WA MAKONDA WAPATA AJALI MASASI

 

MSAFARA wa Katibu wa NEC Itikadi Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Paul Christian Makonda umepata ajali katika Kijiji cha Sululu  wilayani Masasi mkoani Mtwara leo majira ya saa 9 alasiri, ikihusisha zaidi ya magari 7 yaliyokuwa kwenye msafara huo.

Msafara huo ulikuwa ukirejea jijini Dar es Salaam baada ya kusitishwa ziara yake kutokana na kifo cha Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa kilichotokea hapo jana.

Taarifa zilizothibitishwa kutoka eneo la tukio zinaeleza kuwa, watu saba wamejeruhiwa na kukimbizwa katika Hospitali ya Wilaya ya Masasi mkoani Mtwara, lakini hakuna kifo kilichotokea.

Pamoja na ajali hiyo, hali ya Katibu wa Halmashauri Kuu Itikadi, Uenezi na Mafunzo Ndugu Paul Makonda iko salama.

   

No comments