Header Ads

ad

Breaking News

MKOA WA RUVUMA WAKUSANYA MAPATO KWA ASILIMIA 134

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas akizungumza kwenye ufunguzi wa kikao cha RCC Mkoa wa Ruvuma kilichofanyika kwenye ukumbi wa Manispaa ya Songea 

 Na Albano Midelo,Songea

MKUU wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas  ameipongeza Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) kwa kufanikiwa kukusanya mapato ya ndani zaidi ya shilingi bilioni 29.5 sawa na asilimia  134 katika kipindi cha mwaka 2022/2023.

Kanali Thomas ametoa pongezi hizo wakati anazungumza kwenye ufunguzi wa Kikao cha Baraza la Ushauri la Mkoa (RCC) kilichofanyika kwenye ukumbi wa Manispaa ya Songea.

Amesema TRA katika kipindi hicho wamefanya kazi nzuri ya kukusanya mapato kwa kuwa wamevuka lengo la makusanyo ya zaidi ya shilingi bilioni 21 ambapo amesema Uchumi wa Mkoa wa Ruvuma umeendelea kuimarika.

“Mkoa unaendelea kuimarika kiuchumi kwa kuimarika kwa miundombinu,shughuli za uzalishaji mali,biashara na ukewekezaji shughuli za uchimbaji madini hasa makaa ya mawe,maboresho ya uwanja wa Ndege wa Songea na biashara na nchi jirani za Msumbiji na Malawi’’,alisistiza RC Thomas.

Ameyataja mazingira ya kujifunzia na kufundishia  wanafunzi yamekuwa bora zaidi ambapo Mkoa uliletewa fedha za kujenga shule mpya 12 za msingi kupitia BOOST kwa gharama ya zaidi ya shilingi bilioni 7,7 pia serikali ilileta fedha zaidi ya shilingi bilioni tano kujenga sekondari mpya tisa kupitia program ya SEQUIP.

Kulingana na Mkuu wa Mkoa katika kipindi cha mwaka 2022/2023 serikali imetoa shilingi milioni 900 kukarabati hospitali kongwe ya Tunduru na zaidi ya shilingi bilioni tatu zimetolewa na serikali  kujenga hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Ruvuma katika eneo la Mwengemshindo Manispaa ya Songea.

Ameongeza kuwa serikali imetoa shilingi bilioni 9.3 kujenga vituo vya afya 14  na kwamba serikali imenunua mashine ya CT scan na digital xray kwa ajili ya hospitali ya Rufaa ya Mkoa na mashine ya Xray kwa ajili ya hospitali ua Halmashauri ya Madaba.

Akizungumzia sekta ya kilimo,Mkuu wa Mkoa amesema serikali imeingiza mbolea ya ruzuku mkoani Ruvuma jumla ya tani 90,000  ambapo hadi sasa mbolea tani 62,540 zimesambazwa kwa wakulima.

 Maazimio yaliyopitshwa katika kikao hicho cha RCC ni Pamoja na kila halmashauri kutumia mapato yake ya ndani kujenga shule ya bweni ya wavulana na wasichana na kufanya ufuatiliaji wa ujenzi wa chuo cha SUA tawi la Tunduru.

No comments