Header Ads

ad

Breaking News

KIKAO KAZI WADAU HUDUMA ZA SERIKALI MTANDAO CHAHITIMISHWA

Na Mwandishi Wetu

KIKAO kazi cha nne cha wadau wa Huduma za Serikali Mtandao ( e-GA ) kimehitimishwa Februari 8, 2024 katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC), jijini Arusha.

Mgeni rasmi katika tukio hilo, Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Ridhiwani Kikwete amewapongeza waandaaji kwa mafanikio makubwa yaliyopatikana katika siku nne za kikao hicho na kuzitaka taasisi za umma kuongeza matumizi ya Serikali Mtandao katika huduma zake.

Naibu Waziri Kikwete alitembelea mabanda mbalimbali ya maonesho ya wadau wa huduma za Serikali Mtandao, ambapo katika banda la Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), ametoa pongezi kwa mamlaka kuanza kutumia mfumo wa pamoja wa kielektroniki wa uondoshaji wa shehena bandarini 'Single Window System' unaoiunganisha TPA na Mamlaka nyingine zinazohusika katika mnyororo wa huduma za bandari.









No comments