Header Ads

ad

Breaking News

AZAM FC YAILAZIMISHA SIMBA SC SARE YA BAO 1-1

 

Kiungo wa timu ya Simba, Clatous Chama akishangilia baada ya kuisawazishia timu yake bao dhidi ya Azam FC, leo Februari 9,2024 jijini Mwanza.

Na Mwandishi Wetu, Mwanza

SIMBA SC leo Ijumaa Februari 10,2024, imelazimisha sare ya kufungana bao 1-1 na Azam FC, katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara uliopigwa Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

Katika mchezo huo, Azam FC walikuwa wa kwanza kupata bao lililofunga Mzimbabwe Prince Dube dakika ya 14, akiitumia vizuri pasi ya Paschal Msindo, baada ya kazi nzuri iliyofanywa na Yahya Zayd.

Furaha za mashabiki wa Azam FC, zilizimwa dakika ya 90, kwa bao safi la mpira wa adhabu uliopigwa na kiungo Mzambia Clatous Chama, na kujaa wavuni, huku mpira ukimshinda kipa aliyesajiliwa dirisha dogo kutoka Sudan, Mohamed Mustafa.

Kwa matokeo hayo, Azam FC inaendelea kushika nafasi ya pili ikiwa imejikusanyia pointi 32, ikiwa imecheza mechi 14, huku Simba wakiendelea kubaki nafasi ya tatu wakiwa na alama 30, michezo 13. Yanga wanaongoza ligi wakiwa na alama 37, wakicheza mechi 14.

Mshambuliaji wa Azam FC, Prince Dube (kulia), akishangilia bao alilofunga dhidi ya Simba SC, leo Februari 9,2024 kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza. Mwingine ni Pascal Msindo



No comments