Header Ads

ad

Breaking News

Wagumu Group Mdaula yakabidhi vifaa Zahanati

Wana Kikundi cha Wagumu wakiwa katika picha ya pamoja. Picha na Omary Mngindo

Na Omary Mngindo, Mdaula

KIKUNDI cha Wagumu kilichopo Kitongoji cha Mdaula Kata ya Bwilingu Halmashauri ya Chalinze Wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani, kimekabidhi vifaa mbalimbali katika Zahanati ya Mdaula.

Vifaa hivyo ni sabuni za maji za vipande, mifagio, vikinga mikono na vifaa mbalimbali vilivyogharimu zaidi ya shilingi ya milioni moja, huku wadau mbalimbali wakiungana kufanikisha zoezi hilo.

Mwenyekekiti wa kikundi hicho Shabani Athumani alisema wamechukua hatua hiyo ikiwa ni kuunga mkono juhudi za Rais Dkt. Samia Suluhu Hassa za kuhakikisha huduma za afya zinaboreshwa.

"Kikundi chetu kinaundwa na wanachama 22 ambao tunajitolea katika kusaidia jamii katika nyanja mbalimbali ikiwemo kusaidia familia zenye uhitaji, ambapo tunasaidia kidogo kinachokipata," alisema Athumani.

Athumani alisema wapo katika jamii kuisaidia, wana miradi ya bodaboda, wanachomelea, chekechea na shimo la kuchimba madini.

Mwenyekiti wa Kitongoji hicho, Shabani Ally aliwapongeza vijana hao kurudisha kwa jamii kile wanachokipata, huku akimpongeza Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa, pamoja na Mbunge Ridhiwani Kikwete na Diwani Nassa Karama.

"Kikundi hiki kimekuwa msaada katika kitongoji chetu, kimekuwa kikisaidia sekta ya afya, elimu na jamii wakiwemo wazee wasio na uwezo, huku wakimpongeza Rais Samia kwa kazi kubwa, bila kuwasahau Mbunge Ridhiwani Kikwete na Diwani Nassa Karama,"alisema mwenyekiti huyo.

Hosen Mtibu, Katibu wa Wagumu alisema kuwa, wanawafikia vijana na wazee, pia ni mabalozi wa Sekondari ya Msaula, ambapo huwasaidia wanafunzi wenye changamoto za kimaisha.

"Tunasaidia wanafunzi wanaokabiliwa na changamoto katika familia zao, kwa kuwapatia mahitaji muhimu kwa lengo la kuwawezesha kufikia malengo yao ya kielimu," alisema Mtibu.

No comments