Header Ads

ad

Breaking News

Mbunge Mgalu asema madimbwi yatabaki historia Bagamoyo

MBUNGE Viti Maalumu Mkoa wa Pwani, Subira Mgalu akizungumza katika mkutano wa uzinduzi wa Kampeni kwenye Kata ya Nianjema. 

Na Omary Mngindo, Bagamoyo

MBUNGE wa Viti Maalumu Mkoa wa Pwani, Subira Mgalu, amesema mradi wa Taktik unaoboresha miji 30 nchini utaondoa madimbwi katika mji wa Bagamoyo na kubaki historia.

Mgalu aliyasema hayo mwishoni nwa wiki akiwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa mikutano ya hadhara ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Kata ya Nianjema mbele ya Mwenyekiti Omary Makamba, Katibu Mwenezi Minjoli, Diwani Abdul Pyalla, alisema katika mradi huo na Bagamoyo imejumuishwa.

Alisema kuwa, licha ya kazi nzuri inayoonekana ya kupatikana kwa kilometa moja ya lami kwa mara ya kwanza, lakini kupitia mpango uliopo madimbwi katika mji huo yatabaki historia.

"Kama alivyosema diwani na kwa namna anavyosaidiana na mbunge, nami nipo katika Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti, tumeona dhamira ya serikali ya kuboresha miundombinu ya ngazi za mitaa na vitongoji, hususan kwenye miji ya kihistoria," alisema Mgalu.

"Nataka niwatoe hofu, madimbwi yatabaki historia, Serikali imejipanga vizuri ukizingatia Bagamoyo ni mji wa kihistoria na mji wa utalii, safari ya kwanza ya rais kurekodi filamu ya Royal Tour akitokea Zanzibar, kwa upande wa bara ilianzia hapa," alisema.

Aliongeza kuwa, "Tumeona ni namna gani utalii umeongezeka, ninapozungumza zaidi ya watalii 1,700,000 waliingia, ni ongezeko zuri kutoka 1,300,000, hapa Bagamoyo walioongezeka, fedha zilipatikana ni dhahiri kwamba fedha za ujenzi wa miundombinu ya barabara itaendelea kuboreshwa," alisema.

Diwani wa Kata hiyo, Pyalla alizungumzia idadi ya wanafunzi 504 katika kata hiyo wataKaoanza Kidato cha kwanza mwaka huu.

Alisema idadi hiyo ya wanafunzi imetokana na kufauli masomo yao ya shule za msingi zilizopo ndani ya kata hiyo, ambapo wataanza masomo yao kwenye shule ya sekondari iliyopo kwenye kata hiyo.

"Nitumie nafasi hii kuishukuru Serikali inayoongozwa na Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan, tumefanikiwa kupata s ya sekondari katika Kata yetu, hatua ambayo imeokoa watoto wetu waliokuwa wanakwenda kusoma katika shule za mbali, kwa mwaka huu wanafunzi 504 wataanza kidato cha kwanza," alisema Pyalla.

Diwani wa Kata ya Nianjema, Abdul Pyalla akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika kata hiyo. Picha zote na Omary Mngindo.

No comments