Header Ads

ad

Breaking News

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA ARDHI YATEMBELEA KAZI YA UBORESHAJI MFUMO WA SEKTA YA ARDHI



Na Munir Shemweta, WNMM ARUSHA

KAMATI ya Kudumu ya Bunge Ardhi Maliasili na Utalii imetembelea kazi ya Uboreshaji Mfumo Unganishi wa Usimamizi wa Sekta ya Ardhi inayofanywa na timu ya wataalamu mkoani Arusha.

Mfumo huo unatarajiwa kuanza katika mikoa mitano ya Arusha, Dodoma, Mwanza, Mbeya na Tanga na utarahisisha na kuharakisha upatikanaji huduma za sekta ya ardhi kwa kuwa wananchi watakuwa wakipata huduma kwa njia ya mtandao.

Akizungumza wakati wa kuikaribisha Kamati hiyo jijini Arusha tarehe 8 Januari 2023 Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Jerry Silaa amesema, mfumo unaoboreshwa na timu ya wataalamu mkoani Arusha asilimia mia moja utakuwa ni wa kidigitali.

"Baada ya kazi ya maboresho ya mfumo kukamilika, hatua zozote za ardhi zitakuwa zikifanyika kwenye mfumo na suala la mwananchi kwenda ofisi za ardhi kupata huduma ni uamuzi wake mwenyewe,’’alisema Silaa

Mkurugenzi wa Tekonolojia ya Habari na Mawasiliano wa Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Flateny Hassan ameeleza kuwa, uboreshaji wa mfumo unafuatia Wizara ya Ardhi kuwa na changamnoto  kadhaa kwenye mifumo yake jambo alilolieleza kwamba limesababisha kuwepo uhitaji wa kuunganisha mifumo yote ili kuwa na mfumo mmoja utakaohusika na sekta ya ardhi.

‘’Kazi inayofanywa na timu ya wataalam jijini Arusha kwa sasa imefikia asilimia 85 na matarajio ni kwamba ikifika Juni 2024 mikoa ya awali iliyopangwa itakuwa imefikiwa," alisema Flateny

Maboresho yanayofanyika ni pamoja na mfumo unaoruhusu watumishi wa sekta ya ardhi kutekeleza majukumu yao ndani ya ofisi zao, mfumo unaoruhusu wananchi kuomba huduma kwa njia ya mtanadao na huduma ya Mobile App ambao mwananchi anaweza kupata huduma kupitia njia ya mkononi.

Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi imekuwa katika jitihada kubwa za kuhakikisha huduma za sekta ya ardhi zinapatikna kwa haraka na urahisi  kupitia mifumo ya kidigitali.

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Jerry Silaa akizungumza wakati Kamati ya Kudumu ya Bunge Ardhi Maliasili na Utalii ilipotembelea kazi ya Uboreshaji Mfumo Unganishi wa Usimamizi wa Sekta ya Ardhi inayofanywa na timu ya wataalamu mkoani Arusha 

 Sehemu ya wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi Maliasili na Utalii wakifuatilia uwasilishwaji kazi ya Uboreshaji Mfumo Unganishi wa Usimamizi wa Sekta ya Ardhi inayofanywa na timu ya wataalamu mkoani Arusha.

Sehemu ya wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi Maliasili na Utalii wakifuatilia uwasilishwaji kazi ya Uboreshaji Mfumo Unganishi wa Usimamizi wa Sekta ya Ardhi inayofanywa na timu ya wataalamu mkoani Arusha.

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Geophrey Pinda akizungumza wakati Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi Maliasili na Utalii ilipokwenda jijini Arusha kukagua kazi ya Uboreshaji Mfumo Unganishi wa Usimamizi wa Sekta ya Ardhi tarehe 8 Januari 2024.

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii, Timotheo Mzava akizungumza wakati Kamati yake ilipotembelea kazi ya Uboreshaji Mfumo Unganishi wa Usimamizi wa Sekta ya Ardhi inayofanywa na timu ya wataalamu mkoani Arusha, Januari 8,2024

Baadhi ya wataalamu wanaofanya kazi ya kufanya Maboresho Mfumo Unganishi wa Usimamizi wa Sekta ya Ardhi.

Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhandisi Anthony Sanga akizungumza wakati Kamati ya Kudumu ya Bunge Ardhi Maliasili na Utalii ilipotembelea kazi ya Uboreshaji Mfumo Unganishi wa Usimamizi wa Sekta ya Ardhi inayofanywa na timu ya wataalamu mkoani Arusha, Januari 8,2024.

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Jerry Silaa na Naibu wake, Geophrey Pinda wakifuatilia uwasilishwaji taarifa ya kazi ya Uboreshaji Mfumo Unganishi wa Usimamizi wa Sekta ya Ardhi inayofanywa na timu ya wataalamu mkoani Arusha, Januari 8, 2024.(Picha zote na Wizara ya Ardhi)

No comments