Header Ads

ad

Breaking News

Estate mabingwa bonanza la Wagumu

Moja ya mechi iliyochezwa katika bonanza lililoandaliwa na Kikundi cha Wagumu cha Mdaula, Kata ya Bwilingu katika Halmashuri ya Chalinze. Picha na Omary Mngindo.

Na Omary Mngindo, Mdaula

TIMU ya soka ya Ubena Estate inayomilikiwa na Kampuni ya Estate inayojihusisha na kilimo cha mkonge,imetwaa ubingwa wa soka wa michuano iliyoandaliwa na Kikundi cha Wagumu Group cha Mdaula.

Estate imetwaa ubingwa huo baada ya kuichapa Maokoto mabao 2-0, na kukabidhiwa zawadi ya jezi, mshindi wa pili aliondoka na mpira mmoja, huku zawadi mbalimbali zikitolewa kwa wachezaji mbalimbali waliofanya vizuri.

Katika bonanza hilo lililofanyika Uwanja wa Shule ya msingi Mdaula liliandaliwa na kikundi hicho, mbali ya soka michezo mingine iliyofanyika ni netiboli na mpira wavu, huku washindi katika kila mchezo wakiibuka na zawaidi mbalimbali.

Bonanza hilo lililofanyika Januari Mosi, liliambatana na kukabidhi vifaa mbalimbali katika Zahanati ya Mdaula, ikiwa ni kurejesha faida wanayopata kitongojini hapo kutokana na shughuli za kimaendeleo wanazofanya.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya bonanza hilo, Mwenyekiti wa kikindi hicho, Shaban Athumani alisema kikundi chao kilianzishwa mwaka 2018, malengo yake yakiwa ni kuhamasisha michezo kwa vijana.

"Hii leo ni mwendelezo wa shughuli za kimichezo tunazoziandaa wana Wagumu Group, pia tunasaidi timu mbalimbali zinapopata mialiko ya kimichezo iwe ndani ya wilaya au nje ya mkoa wetu, tunachangia kusafirisha timu," alisema Athumani.

No comments