Header Ads

ad

Breaking News

YANGA ANGA NYINGINE, YAIPIGA SIMBA 5G

Wachezaji wa Yanga wakishangalia kwa kuonesha vidole vitano

Na Mwandishi Wetu
YANGA wamedhihirisha ubora wao, wamedhihirisha sababu ya kuingia kwenye kinyang'anyiro cha tuzo ya timu Bora barani Afrika, baada ya kuibamiza Simba mabao 4-1.

Mchezo huo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara, uliopigwa Uwanja wa Benjamini Mkapa jijini Dar es Salaam, ulishuhudia Yanga wakipata bao la kwanza la mapame zaidi dakika ya tatu, lililofungwa na Kennedy Musonda kwa kichwa.

Hata hivyo, Kibu Denis alirejesha furaha kwa wana Msimbazi, Simba, baada ya kuisawazishia bao hilo dakika ya nane, tena kwa kichwam kama lilivyokuwa la watani wao wa jadi.

hata hivyo Yanga walidhihirisha ubora wao baada ya kupata bao la pili dakika ya 64, lililokwamishwa wavuni na Maxi Nzengeli. Bao hilo liliwaongezea morali baada ya Nzengeli kuongeza bao la tatu dakika ya 77, akiwazidi ujanja mabeki wa Simba, Henock Inonga na Che Fondoh Malone.

Pamoja na jitihada za Simba kusaka bao la kusawazisha, walijikutaka wakichapwa bakora ya nne dakika ya 73, lilikwamishwa wavuni na Stephane Aziz Ki, lakini bao lililowamaliza nguvu kabisa ni lile lililofungwa na  Pacome Zouzoua dakika ya 87.

Kwa matokeo hayo, Yanga wamekaa kileleni mwa msimamo wa Lighi Kuu ya NBC baada ya kujikusanyia alama 21, huku Azam FC ikiwa nafasi ya pili na alama zake 19, huku Simba wakiwa na alama 18.
Kibu Denis akifunga bao la kusawazisha kwa kichwa
Maxi Nzengeli (aliyepiga magoti), akishangilia bao alilofunga. Kushoto ni Dickson Job na Mahlatse Makudubela

Kiungo mshambuliaji Stephane Aziz Ki, akishangilia kwa kuonesha fulana yenye maandishi 'Happy Birthday Chiocharito'
Kiungo Pacome Zouzoua 'Profesa' akimtoka Mwamba wa Lusaka, Clatous Chama
 Profesa wa mpira, pacôme zouzoua (katikati), akipongezwa baada ya kuifungia timu yake ya Yanga bao la tano 
Kiungo mshambuliaji wa Yanga, Stephane Aziz Ki akiwa katikati ya msitu wa mabeki wa Simba, Che Malone, Shomary Kapombe, Henock Inonga na Sadio Kanoute
Stephane Aziz Ki (kulia) na Henock Inonga wakiwania mpira

Beki wa Simba, Che Malone akimdhibiti Kennedy Musonda, katika mechi ya Ligi Kuu ya NBC iliyopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam. Yanga wameibuka na ushindi wa mabao 5-1

 Mshambuliaji wa Simba, Kibu Denis, akiwatoka wachezaji wa Yanga, Joyce Lomalisa (kulia), Stephane Aziz Ki (wa kwanza kushoto) na Maxi Nzgengeli
Kibu Denis akishangilia baada ya kuisawazishia timu yake ya Simba bao la kwanza dhidi ya Yanga. Simba walipoteza kwa kupigwa mabao 5-1.

No comments