WCF IMELIPA MADAI SHILINGI BILIONI 65.34-Dkt Mduma
Na Mwandishi Wetu
MFUKO wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), umelipa madai mbalimbali ya wafanyakazi kiasi cha shilingi bilioni 65.34, malipo hayo niya hadi Septemba 2023.
Hayo yameelezwa na Mkurugenzi wa WCF, Dkt.John Mduma, katika kikao kazi na wahariri na waandishi wa habari kilichofanyika Novemba 2, 2023 jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi huyo amesema kuwa, madai yaliyopokelewa katika kipindi hicho yalikuwa 18,782, yaliyoshughulikiwa yalikuwa madai 14,087 sawa na asilimia 75.
"Tulipokea madai 18,782, kwa suhirikiano wetu yulifanikiwa kushughulikia madai 14,087, sawa na asilimia 75, katika madai hayo, yaliyolipwa ni 12,339, yaliyokataliwa ni 1,440 na madai 308 yamefungwa," amesema.
Amesema kwa upande wa pensheni madai ni 1,466, wenye ulemavu zaidi ya asilimia 30 wako 358, wanaohitaji wasaidizi ni 18, wategemezi 1,090, wakati wanafunzi wako 26.
Mkurugenzi huyo amesema kuwa, kwa upande wa mafao ya wategemezi, hulipwa kihirakia ukianza na mwenza, watoto au wazazi, ambapo mwenza hulipwa asilimia 40 ya mshahara ghafi kwa maisha yake yote.
Amesema kiwango cha chini ni shilingi 110,281.13 kwa mwezi, watoto hupata asilimia 20, lakini hubadilika wanapozidi watatu, ambapo wakifikia miaka 18 ndipo huanza kulipwa au kumaliza elimu ya sekonadri au chuo.
"Tunapunguza umaskini, tunaondoa migogoro, tunaleta utulivu na pia tunaongeza ari ya kazi na mahusiano bora kazini," amesema.
Kuhusu anayemhudumia mgonjwa, Mkurugenzi huyo amesma kuwa, hulipwa kwa mfanyakazi asiyeweza kumudu kujihudumia, hulipwa asilimia 40 ya pensheni ya mfanyakazi, huku msaidizi huteuliwa na mfanyakazi.
"Kuna mafao ya anayemhudumia mgonjwa hulipwa kwa mfanyakazi asiyeweza kumudu kujihudumia, atalipwa asilimia 40 ya pensheni ya mfanyakazi, ambapo msaidizi huteuliwa na mfakazi," amesema.
MKurugenzi huyo amesema kuwa, kwa upande wa mafao ya ulemavu wa kudumu, hulipwa asilimia 70 ya mshahara ghafi mara kiwango cha ulemavu, ambapo kiwango cha chini ni shilingi 275,702.83.
"Ulemavu usiozidi asilimia 30, hulipwa kwa mkupuo, wakati ulemavu unaozidi asilimia 30, hawa hulipwa kwa pensheni kwa maisha yote," amesema.
Ameongeza kuwa, mfanyakazi anapopata ulemavu wa muda na kupewa mapumziko zaidi ya siku tatu au kazi nyepesi, hulipwa asilimia 70 ya mshahara ghafi ambapo kiwango cha chini ni shilingi 275,702.83, hulipwa kwa muda wa miezi 24.
"Hakuna sababu ya kumsimamisha kazi mtumishi aliyepata ugonjwa au ajali ya kikazi chini ya miezi 24, mwajili anaweza kumwajili mtumishi mwingine kwa muda," amesema mkurugenzi huyo.
Kuhusu mafao ya matibabu, amesema huanza kulipwa mara ajali inapotokea, ambapo aina zote zote za matibabu hutolewa bila kujali kiwango cha uchangiaji.
Ameongeza kuwa,mfumo wote wa matibabu Tanzania Bara kwa jupoande wa bima na watoa huduma za afya, hutoa huduma kwa wateja wote wa WCF.
"Mafao ya matibabu kwa upande wetu hakuna ukomo wa gharama na hakuna kifurushi cha matibabu, lengo letu ni kulinda nguvu kazi, kuondoa migogoro, lakini pia tunaleta utulivu," amesema.
Mkurugenzi huyo amesema kuwa, WCF wajibu wake mkuu ni kulipa fidia stahiki kwa wafanyakazi wanaopata ajali au ugonjwa unaotokana na kazi na kwa wategemezi wa wafanyakazi wanaofariki dunia kutokana na kazi.
Katika kutekeleza hilo, WCF inalinda nguvu kazi ya Taifa, inapunguza umaskini na kusaidia kuondoa migogoro kati ya waajiri na wafanyakazi hasa mfanyakazi anapopata ajali au ugonjwa unaotokana na kazi.
Ameongeza kuwa, wajibu mwingine wa WCF ni kuwawezesha waajiri kutekeleza majukumu yao ya uzalishaji badala ya kushughulikia madai ya faida, huku ikisaidia kuleta uelewani na utulivu katika jamii.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Dkt.John Mduma akiteta jambo na Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Deodatus Balile.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusaino Ofisi ya Msajili wa Hazina, Thobias Makoba.
No comments