Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi waimarika kifedha
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Dkt. John Mduma akizungumza katika kikao kazi kati ya mfuko huo, Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) na Ofisi ya Msajili wa Hazina kilichofanyika kwenye Ofisi za Mfuko huo Victoria jijini Dar es Salaam.
Na Mwandishi Wetu
MKURUGENZI Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Dkt.John Mduma amesema wamefanikiwa kuimarika uwezo wa kifedha wa mfuko kwa shilingi bilioni 697.83 kwa mujibu wa hesabu za mpaka Septemba 30,2023.
Hayo yameelezwa na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko huo, wakati akizungumza na wahariri na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali katika mkutano wa kikao kazi ulioratibiwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina.
MKurugenzi huyo amesema idadi ya madai ya fidia kwa wanufaika yaliyopokelewa na mfuko watehama ni 18,782, wakati jumla ya madai 14,087 yameshughulikiwa na madai 12,339 yamelipwa, madai 1,440 yamekataliwa na 308 yamefungwa.
Amesema kuwa, ulipaji wa fidia kwa wanufaika umeongezeka kutoka kulipa shilingi bilioni 1.55 mwaka 2017 hadi kufikia kulipa shilingi bilioni 65.35 mwaka 2023.
"Tumefanikiwa kuboresha huduma kupitia usimikaji mifumo ya TEHAMA, Kuboresha kwa kituo cha huduma kwa wateja na kuboresha tathmini za ulemavu kupitia mafunzo kwa madaktari,"amesema.
Dkt.Mduma amesema Kwa upande wa ukusanyaji michango waajiri wote wanatakiwa kuchangia mfuko huo, ambapo hadi sasa umefanikiwa kulipa kiasi cha shilingi bilioni 65 kwa wanufaika wake na kuahidi kuuimarisha zaidi kwa maslahi ya watanzania na taifa.
"Mfuko hadi sasa umetoa malipo ya Kodi ya serikali inayotokana na mapato kiasi cha shilingi bilioni 62.7, hadi kufikia Septemba 2023 mfuko umesajili asilimia 93 ya wanufaika," amesema.
Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Deodatus Balile, amewataka wahariri na waandishi wa habari kuhakikisha wanafikisha taarifa kwa waajiri wao ili wapate haki yao ya msingi ya kujiunga na mfuko huo.
Balile amewataka mashuhuda waliopata changamoto na kulipwa fidia zao kuwa tayari kuzungumza na vyombo vya habari ili kama mabalozi ili elimu kuhusu Mfuko iwafikie wananchi wengi.
Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) Anselim Peter, akizungumza katika kikao kaziMkurugenzi wa Huduma za Tathmini wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Dkt. Abdulsalaam Omar akieleza jambo kwenye kikao kazi
Afisa Mawasiliano Ofisi ya Msajili wa Hazina, Sabato Kosuri, akizungumza katika kikao kazi
Wahariri na waandishi wa habari wakimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Mfuklo wa Fidia kwa Watumishi (WCF), Dkt.John Mduma.
Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano Ofisi ya Msajili wa Hazina, Thobias Makoba (kushoto), akizungumza jambo na Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Deodatus Balile katika kikao kazi kilichofanyika leo Alhamisi Novemba 2,2023.
No comments