Header Ads

ad

Breaking News

KOCHA BORA WA OKTOBA ATIMULIWA KAZI, MATOLA AREJEA SIMBA

Kocha Oliveira Gonçalves do Carmo 'Robertinho' 

Na Mwandishi Wetu
MABINGWA wa Ngao ya Hisani, Simba SC, imefuta kazi kocha  wao Mbrazil, Roberto Oliveira Gonçalves do Carmo 'Robertinho' (63), baada ya kipigo cha mabao 5-1 dhidi ya watani wao wa jadi Yanga.

Miamba hiyo ilikutana katika mchezo wa derby Ligi Kuu ya NBC mwishoni mwa wiki, ambapo Yanga waliibuka kinara baada ya kuigagadua DSimba mabao 5-1.

 Robertinho ameiongoza timu hiyo miezi 10 tu, tangu alipolamba mkataba Januari 13, mwaka huu, akitokea Vipers ya Uganda, huku Simba ikitoa taarifa ya kuachana naye jana mchana.

Katyika taarifa, Simba imesema pamoja na Robertinho, ataondoka na Kocha wa viungo, Cornoille Hategekimana raia wa Rwanda, hivyo timu itakuwa chini ya Daniel Cadena kutoka Hispania.

 Cadena alikuwa kocha wa makipa ambaye atafanya kazi kocha wa timu za vijana, Suleiman Matola., huku mashabiki wa soka wakitafsiri kwamba, kipigo cha Yanga kwenye Uwanja wa Benjamini Mkapa jijini Dar es Salaam ndicho kilichosababisha kumfuta kazi kocha huyo.

Mabao ya Yanga yalifungwa na Kennedy Musonda dakika ya tatu, Maxi Nzengeli dakika ya 64 na 77, Stephane Aziz Ki dakika ya 73 na Pacome Zouazoua dakika ya 87 kwa mkwaju wa penalti, wakati bao la simba lilifungwa na Kibu Dennis dakika ya tisa. 

 Yanga SC imejikusanyia pointi 21, baada ya kucheza mechi nane na kukaa kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu, ikifuatiwa na Azam FC yenye pointi 19, huku Simba ikishuka hadi nafasi ya tatu ikiwa imejikusanyia alama  18.





No comments