Header Ads

ad

Breaking News

Kilometa za mraba 534,000 zimefanyiwa utafiti mafuta, gesi-Mhandisi Sangweni

Mkurugezi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA), Mhandisi Charles Sangweni akizungumza na wahiriri na waandishi wa habari (hawapo pichani), katika kikao kazi kilichofanyika leo Jumatatu Novemba 6,2023.

Na Frank Balile

MKURUGENZI Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA), Mhandisi Charles Sangweni amesema kilometa za mraba 534,000 zimefanyiwa utafiti wa upatikana kwa mafuta na gesi asilia.

Mhandisi Sangweni amesema kuwa, kilometa za mraba 394,000, utafiti wake umefanyika nchi kavu na kilomita za mraba 140,000, utafiti wake umefanyika upande wa baharini.

Amesema maeneo mengi yamefanyiwa utafiti wa awali ambapo data, taarifa na takwimu zake zipo (Gravity/magnetic and 2D SEISMIC), huku akiweka wazi kwamba, hadi Sasa gesi asilia iliyogunduliwa nchi kavu na kina kirefu cha bahari ni futi za ujazo trilioni 57.54.

Mhandisi Sangweni amesema kuwa, kwa upande wa nchi kavu ni futi za ujazo trilioni 10.41, wakati baharini gesi iliyogunduliwa ni futi za ujazo trilioni 47.13.

Mhandisi Sangweni ameeleza hayo leo Novemba 6,2023 jijini Dar es Salaam wakati wa kikao kazi kati ya PURA, wahariri na waandishi wa habari, kikiwa kimeratibiwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina.

Amesema visima vya Utafutaji wa mafuta vilivyochimbwa nchi kavu ni 59, na visima 37 vikiwa eneo la baharini, wakati gesi asilia imegunduliwa kwenye visima 44, kati ya visima 96 vilivyochimbwa.

"Kati ya visima 44 vilivogundulika kuwa na gesi, visima 16 vilichimbwa nchi kavu na 28 vilichimbwa baharini,"n amesema Mhandisi Sangweni.

Ameyataja maeneo yaliyogunduliwa gesi asilia ni Songosongo mwaka 1974, Mnazi bay mwaka 1982, Mkuranga mwaka 2007, Kiliwani Kaskazini mwaka 2008, Ntorya mwaka 2012, Ruvu mwaka 2016, wakati kina kirefu cha bahari ni kaunzia mwaka 2010.

Mhandisi Sangweni amesema kuwa, kwa sasa wastani wa uzalishaji gesi asilia umeongezeka na kufikia Futi za ujazo bilioni 53.19, katika Kipindi cha Julai 2022 hadi Februari 2023 ikilinganishwa na futi za ujazo bilioni 46.96 mwaka 2021/2022 sawa na Ongezeko la asilimia 14.

Amesema uzalishaji gesi asilia umesaidia kutumika kuzalisha umeme, matumizi ya magari, majumbani na viwandani, kwani  gesi iliyozalishwa imechangia asilimia 70 ya umeme unaopatikana nchini.

Mkurugenzi Mkuu huyo amesema, PURA ilianzishwa miaka nane iliyopita inatekeleza majukumu yake kama yalivyoainishwa kwenye Sheria ya Petroli 2015, kifungu cha 12.

Afisa Uhusiano Mwandamizi, Ofisi ya Msajili wa Hazina (TR), Sabato Kosuri, akiongoza kikao hicho.
Wahariri wakisikiliza maelezo kutoka kwa M kurugenzi Mkuu, Mhandisi Charles Sangweni (hayupo pichani)

Maafisa wa Mamlaka ya Udhibiti Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA), akisikiliza kwa makini

Baadhi ya Wahariri waliohudhuria

                                            Wahariri wakifuatilia maelezo ya kikao kazi
Msimamizi Mkuu wa Blog ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bashir Nkoroma, akiuliza swali katika kikao kazi kilichofanyika leo Jumatatu Novemba 6,2023






No comments