Header Ads

ad

Breaking News

EWURA YAWEKA MIKAKATI KUIMARISHA SEKTA YA MAFUTA, MAJI

Mkurugenzj Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), James Andilile (kushoto), akizungumza kwenye kikao kazi, pembeni yake ni Meneja Mawasiliano na Uhusiano wa mamlaka hayo, Titus Kaguo.

Na Frank Balile

MKURUGENZI Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), James Andilile amesema serikali imejipanga kuhakikisha sekta ya maji inazidi kuimarika na kupatikana nchini kote.

Andilile ametoa kauli hiyo Novemba 6,2023 jijini Dar es Salaam wakati wa kikao kazi na wahariri na waandishi wa habari, kwamba serikali imejiwekea mikakati ya kuhakikisha ifikapo 2025 asilimia 95 ya watu wanaoishi mjini wanafikiwa na huduma ya maji safi na salama.

Amesema mbali na wakazi wa mijini, pia watahakikisha vijijini mtandao wa maji utakuwa umefikia asilimia 85, lakini hadi sasa kwa upande wa mijini yamefikiwa asilimia 88 na vijijini silimia 77.

“Kwa mwaka jana miezi kama hii tulikua na mgogoro wa maji lakini serikali ikachukua hatua ikiwemo kuchimba visima virefu kwenye maeneo mbalimbali”amesemaAndilile.

Amesema serikali ilichimba visima virefu Kimbiji Bagamoyo vyenye thamani ya shilingi bilioni 46 na Mkuranga shilingi bilioni 6 ili kuwewawezesha wananci upatikanaji wa maji.

Mkurugenzi huyo amesema kwa Jiji la Dar es Salaam, kuna miradi mikubwa  inaendelea kutekelezwa likiwemo bwawa kubwa la Kidunda ambalo ujenzi wake hadi sasa umefikia asilimia 10.

"Tunapambana kuhakikisha Dar es Salaam inaondokana na kero ya maji, kwasasa kuna miradi mikubwa ya maji inaendelea kujengwa likiwemo Bwawa la Kidunda ambalo ujenzi wake kwa sasa umefikia asilimia 10,"amesema.

Mkurugenzi mkuu huyo amesema visima vilivyochimbwa maeneo ya Kimbiji na Mkuranga, vimesaidia kuondoa upungufu wa maji uliokuwepo miaka ya nyuma, na kwamba miradi hiyo ya maji inatekelezwa kwenye majiji ya Arusha na Mwanza.

Amesema Bwawa lingine kubwa la Kwakwa limejengwa jijini Dodoma, huku serikali ikiendelea na utoaji wa maji kutoka Ziwa Victoria na kuyapeleka  Dodoma na mikoa mingine.

Andilile amesema kwa kushirikiana na mamlaka za maji, wanaendelea kufuatilia upatikanaji wa maji, ambapo mpaka sasa wanasimamia mamlaka 85, lengo likiwa ni kuhakikisha huduma wanazotoa zinakua bora na zenye viwango vinavyotakiwa.

Kwa upande wa sekta ya umeme, Mkurugenzi mkuu huyo amesema serikali inaendelea kuwekeza katika miradi mbalimbali ili kuhakikisha nchi inakua na umeme wa uhakika.

Andilile amezungumzia mradi mkubwa wa wa kufua umeme wa wa Bwawa la Julius Nyerere  ambao umekamilika kwa asilimia 90, utakaozalisha megawati 2,515 na mradi wa Kinyerezi 1 wenye uwezo wa kuzalisha megawati 185, lakini hivi sasa unazalisha megawati 180.

"Mbali miradi hiyo, pia kuna mradi wa Rusumo unaozalisha megawati 87 ambazo zimefanywa kwa ushirikiano serikari ya Tanzania, Burundi na Rwanda, ambao umekamilika kwa asilimia 99, nchi yetu inapata megawati 26.7 za umeme ambazo zimeingizwa kwenye gridi ya Taifa.

Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Deodatus Balile, ameishauri EWURA wanapotoa leseni za biashara ya vituo vya mafuta, wahakikishe wanaweka pampu moja ye mfumo wa gesi.

Amesema hivi sasa upatikana na wa gesi ya kwenye magari umekuwa mgumu kutokana na vituo vinavyotoa huduma hiyo kuwa vichache, lakini kama EWURA wakitumia njia hiyo itasaidia magari mengi kuwekwa mfumo wa kutumia gesi ambao hauna gharama na pia ni rafiki wa mazingira.

Ameishukuru EWURU kwa kuendesha kikao kazi hicho kilichokuwa na lengo la kufahamiana na kuelezana majukumu yanayofanywa na mamlaka hayo.

 Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), James Andilile (kushoto), akimkabidhi Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (EWURA), Deodadus Balile jarida jipya la utafiti kwa wateja wao.
Wahariri wakifuatilia wasilisho la Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, James Andilile (hayupo pichani), katika kikao kazi
Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Salim S.Salim (kushoto), Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), James Andilile (katikati) na Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Deodatus Balile, wakisikiliza maswali na maoni kutoka kwa wahariri na waandishi wa habari.

         Wahariri wakisikiliza kwa makini
         Wahariri wakisikiliza kwa makini
Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Deodatus Balile na Afisa Habari Mwandamizi Ofisi ya Msajili wa Hazina, Sabato Kosuri (kulia), wakifuatilia taarifa katika kikao kazi
Meneja Mawasiliano na Uhusiano wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), Titus Kaguo (kulia), akieleza lengo la kikao kazi.Katikati ni Mkurugenzi Mkuu wa mamlaka hayo, James Andilile na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Salim S.Salim.

No comments