DKT. SAMIA AMWAGA ZAIDI YA BILIONI MOJA KUTEKELEZA MIRADI ITIGI
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Itigi, Hussein Simba, akiongoza kikao cha robo ya kwanza cha Baraza la Madiwani kilichoketi Oktoba 31, 2023. Kutoka kushoto ni Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Manyoni, Leila Sewa, Mkurugenzi wa halmashauri hiyo, John Mgalula na Naibu Mwenyekiti wa halmashauri hiyo
Na Dotto Mwaibale, Singida
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan amekabidhi takribani Sh.Bilioni 1.6 kwa ajili ya kukamilisha miradi ya sekta ya afya na elimu katika Halmashauri ya Wilaya ya Itigi mkoani Singida.
Hayo yamebainishwa Oktoba 31, 2023 kupitia kikao cha roboya kwanza cha Baraza la madiwani cha kujadili mambo mbalimbali ambacho kilikuwa na ajenda nane.
Akitoa mchanganuo wa matumizi ya fedha hizo Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Hussein Simba alisema katika fedha hizo sh.milioni 700 zinakwenda kutumika kununua vifaa tiba.
Alisema fedha nyingine sh.milioni 100 zinakwenda kujenga zahanati mbili na hivyo kuongeza idadi ya ujenzi wa zahanati hizo kufikia nane na kuwa sh.milioni 500 ambazo zitajenga hospitali ya wilaya, zitatumika kujenga jengo la kufulia, jengo la dawa na la mionzi.
Simba aliongeza kuwa sh.milioni 180 zinakwenda kujenga shule 10 kongwe na sh.milioni 128 zinakwenda kujenga bweni kwa ajili ya watoto wenye mahitaji maalumu.
Alisema sh.milioni 544 zinakwenda kujenga Shule ya Sekondari ya Majengo na zitakazosalia zitatumika kwa ajili ya ujezi wa matundu 20 ya vyoo.
Aidha, Simba alisisitiza kwamba halmashauri hiyo imekuwa ikikusanya mara dufu zaidi ya mapato ikilinganishwa na awali ambapo mpaka sasa kiasi kilicho kusanywa kinafikia asilimia 54 na kuwa matarajio yao hadi itakapofikia robo ya tatu watafikisha asilimia 100.
Simba alipongeza juhudi za Serikali kupitia Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan namna ambayo imeonesha ushirikiano uliotukuka kwa halmashauri hiyo katika muktadha chanya wa ustawi wa maendeleo ya watu.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Manyoni, Leila Sawe na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa wilaya hiyo, Jumanne Ismail walisisitiza halmashauri hiyo kusimamia ipasavyo matumizi ya fedha zote zinazotolewa na Serikali na wadau wa maendeleo kuhakikisha utekelezaji wa miradi unafanyika kikamilifu kulingana na matumizi yaliyopangwa.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Itigi, John Mgalula akizungumza kwenye kikao hicho alipokea ombi la Diwani wa Kata ya Rungwa, Said Yahaya ambaye aliomba asilimia 40 ya mapato yanayokusanywa katika halmashauri hiyo yawe yanapelekwa kwenye kata kwa ajili ya kutekeleza miradi inayoibuliwa na wananchi.
Ametolea mfano wa stendi ya mabasi ya kata hiyo, ambapo alkisema kuwa, jambo hilo litapitiwa kwenye kamati ya fedha kuona namna ya kufanya na kueleza kuwa kabla ya kamati hiyo kukaa, atawatuma madiwani wa viti maalumu kwenda kuangalia mradi huo.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Itigi, John Mgalula akizungumza.
Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Manyoni, Leila Sewa, akizungumza.
Katibu wa CCM Wilaya ya Manyoni Maimuna Likunguni, akichangia jambo.
Diwani wa Kata ya Mgandu, Martin Kapona,akisoma taarifa ya kamati ya fedha.
Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili, William Masaka, akiwasilisha taarifa ya kamati hiyo.
Picha namba 10
Viongozi wakiwa meza kuu wakati wa kikao hicho.
Wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama wakiwa kwenye kikao hicho
No comments