Header Ads

ad

Breaking News

Diwani Gelegeza awaita Bagamoyo Sugar Mkange

Wakazi wa Kata ya Mkange wakichimba msingi wa ujenzi wa shule hiyo


Na Omary Mngindo, Matipwili
DIWANI wa Kata ya Mkange halmashauri ya Chalinze Bagamoyo Mkoa wa Pwani Mohamed Gelegeza, ameuita uongozi wa Kampuni ya Baagamoyo Sugar kwenda kuwekeza katika kata hiyo.


Gelegeza ametoa rai hiyo hivi karibuni wakati wa mahafari ya wahitimu wa kidato cha nne katika Shule ya Sekondari Matipwili, chini ya Mkuu wa Shule, Benjamen Nyamatwema uliualika uongozi wa kampuni hiyo kuwa mgeni rasmi.

"Niwapongeze walimu chini ya mkuu wenu Benjamen Nyamatwema, kwa kuwaalika ndugu zetu wa Bagamoyo Sugar, nami nitumie fursa hii kuuomba uongozi wa Bagamoyo Sugar mje Kata ya Mkange kuwekeza," alisema Gelegeza.

Aliongeza kwamba, katika kata hiyo yenye vijiji vya Saadan, Mandamazingara, Gongo, Mkange na Matipwili kuna fursa nyingi za uwekezaji, hivyo amewaomba kufika katika vijiji hivyo kujionea fursa hiyo.

"Nipelekee salaam kwa viongozi wako wa juu, waambie kwanza tunawashukuru kwa kukubali ombi letu la kuja kuwa mgeni rasmi, tufikishie salaam zetu hizo, pili waambie wana Mkange tunawahitaji waje kuwekeza," alisema. Gelegeza.

Mmoja wa wakazi maarufu katika kata hiyo alisema kijiji cha Matipwili kilitenga ekari 100 kwa ajili ya ujenzi wa shule ya sekondari na kwamba hadi sasa iliyotumika haijafikia hata nusu yake.

"Hapa Matipwili tunazo ekari za kutosha, tunatamani kujenga Chuo cha Maendeleo (VETA), kitachowasaidia watoto wetu kijiendeleza kiufundi ili hata Bagamoyo watakapotangaza nafasi za ajira wapatikane vijana wetu wenye sifa," alisema.
Diwani Kata ya Mkange, Mohamed Gelegeza 

No comments