Header Ads

ad

Breaking News

YANGA YASONGA MBELE HATUA YA MAKUNDI LIGI YA MABINGWA AFRIKA


Na Mwandishi Wetu

MABINGWA wa  soka Tanzania Bara, Yanga, wamesonga mbele hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, baada ya kuibuka na ushindi wa jumla wa mabao 3-0, dhidi ya Al Merreik ya Sudan.

Yanga leo Septemba 30,2023, imeibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Al Merreikh ya Sudan, katika mchezo uliopigwa Uwanja wa Azam Complex jijini Dar es Salaam.

Bao pekee katika mchezo wa leo, limefungwa na Clement Mzize, dakika ya 66 kwa kichwa, akiunganisha mpira wa krosi uliopigwa na Joyce Lomalisa kutoka upande wa kushoto wa uwanja huo.

Katika mchezo wa kwanza ulipopigwa kwenye Uwanja wa Pele pale Kigari nchini Rwanda, Yanga wakiwa ugenini waliibuka na ushindi wa mabao 2-0, hivyo kwa ushindi wa leo wamesonga mbele kwa jumla ya mabao 3-0.

Yanga kutinga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika ilikuwa mwaka 1998,  walipozifunga timu ya Rayon Sport ya Rwanda na Coffee ya Ethiopia katika katika raundi mbili za awali.

Mabingwa hao wa Tanzania, safari yao ilianza kwa kuifunga ASAS ya Djibout na  Al Merreikh ya Sudan.





No comments