WAZIRI MAVUNDE AIBUKIA MKOANI MBEYA, KILOGRAMU 6.93 ZA DHAHABU ZAKAMATWA ZIKITOROSHWA CHUNYA
MADINI yenye thamani ya shilingi milioni 961 zenye uzito wa kilogramu 6.93 yenye thamani ya shilingi milioni 961 yakamatwa wilayanio Chunya mkoani Mbeya yakitoroshwa kwenda kuuzwa nje ya nchi.
Hayo yamebainishwa leo Oktoba 28, 2023 na Waziri wa Madini, Anthony Mavunde, akiwa katika ziara ya kikazi mkoani Mbeya katika machimbo ya dhahabu wilayani Chunya.
Mhe.Mavunde amesema dhahabu iliyokamatwa ina thamani ya zaidi shilingi za kitanzania milioni 961ambapo kama ingetoroshwa Serikali ingekosa mapato ya zaidi milioni 68.
Akizungumza na wafanyabiashara wa madini katika soko la madini Mbeya, Waziri Mavunde amewataka wafanyabiashara wote wa madini kutojihusisha na njama zozote za utoroshaji madini kwani kufanya hivyo, kunakosesha mapato ya nchini na kudumaza juhudi za kuleta maendeleo.
“ Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameonesha dhamira ya dhati ya kuikuza sekta hii ya madini, hivyo ni wajibu wetu kuhakikisha tunafanya biashara hii kwa uadilifu, uaminifu na uzalendo mkubwa na pia kwa kuzigangatia."
Wafanyabiashara wa madini amewataka kuacha kujihusisha na utoroshaji wa madini, huku akiwaeleza wazi kuwa, watachukua hatua kali kwa watu wote wanaohusika bila kusita.
"Niushukuru uongozi wa Mkoa wa Mbeya chini ya Mkuu wa Mkoa, Juma Homera na uongozi wa Wilaya ya Chunya kwa ushirkiano mkubwa wanaotoa kudhibiti utoroshaji”Alisema Mavunde
Naye, Mkuu wa Wilaya ya Chunya *Mayeka S. Mayeka* amesema kuwa mazingira ya uchimbaji madini wilayani Chunya yanaendelea kuhimarishwa hisipokuwa changamoto kubwa ni utoroshaji madini na wizi wa carbon katika mialo ya uchenjuaji.
Awali, akitoa taarifa kuhusu sekta ya madini wilayani Chunya, Afisa Madini Mkazi, Sabahi Nyansiri, alisema hadi sasa vituo vidogo vya ununuzi wa dhahabu ni 24, ambavyo vimefunguliwa ili kusogeza huduma ya ununuzi na uuzaji kwa wachimbaji wadogo wasio na uwezo wa kufika katika soko kuu pamoja na wale wenye kiasi kidogo cha dhahabu.
Katika ziara hiyo Mhe.Mavunde amekagua machimbo ya wachimbaji wadogo wa Itumbi na kufanya mkutano kwa lengo la kujua changamoto zinazowakabili.
No comments