Wanawake wafanyabishara wapewa semina elekezi
TANZANIA Women Chamber of Commerce kwa kushirikiana na East African Women in Business Platforms, leo Oktoba 26,2023 imeendesha semina elekezi kwa wanawake wafanyabiashara katika kuona fursa za kibiashara katika mashirikisho kama vile EAC na AfCFTA.
Semina hiyo ilifunguliwa na Victoria Mwanukuzi, ambayen ni Mkurugenzi TWCC, amesema Semina hiyo iliongozwa na wataalamu wa kibiashara Afrika Mashariki, Dkt. Seth Ogor kutoka nchini Kenya na Adrian Njau wa Trade & Policy Advisor, kutoka Tanzania.
Wanawake walipata kufahamu soko la biashara kwenye mashirikisho tajwa na namna ya kuelewa kupambana na changamoto na faida ya kufanya biashara kwenye mashirikisho hayo.
Semina hiyo ilizingatia kuwajengea uwezo wanawake wafanyabiashara na wajasiriamali kwenye kuelewa ushindani wa soko la kimataifa na namna wanayoweza kuboresha biashara zao.
No comments