Header Ads

ad

Breaking News

Trust St.Patrick yafanya mahafali ya 15 kidato cha nne, 21 darasa la saba

Na Mwandishi Wetu

SHULE ya Sekondari ya Trust St.Patrick ya jijini Arusha, imefanya mahafali ya 15 ya wanafunzi wanaomaliza kidato cha nne mwaka huu Septemba 23,2023, huku darasa la saba ikiwa ni miaka 21.

Akizungumza kwenye mahafali hayo yaliyofanyika Septemba 23,2023 Shuleni hapo, Mkurugenzi wa shule hiyo, Patrick Khanya, amesema kuwa, wanaishuru Serikali kwa kuendelea kuwa na shule binafsi ikiwa lengo ni kutoa elimu bora kwa wanafunzi nchini.

“Naishukuru serikali kwa kuwa bega kwa bega na shule za binafsi, hii ni katika kuona tunapambana ili kutoa elimu bora zaidi na ndiyo maana tunaajiri walimu wenye uweledi wa kutosha na taaluma ya kiwango cha juu ili tupate wanafunzi bora zaidi wenye ufaulu katika masomo na stadi za kazi ambazo zitamwezesha kuwa na ujuzi wa kufanya kazi ya kujiajiri atakapomaliza masomo yake.

“Hivyo basi tunawaomba wazazi na walezi kuwaleta watoto wao katika shule yetu ili waweze kupata elimu bora zaidi ambayo itawasaidia katika kupambana na soko la ajira,”amesema.

Naye, Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Neduvoto Manase , amewashukuru watu wote waliohudhuria mahafali hayo, huku akiwaahidi kufanya vizuri zaidi kitaaluma kwa mwaka huu.

“Namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutufikisha siku hii muhimu na pia namshukuru mkurugenzi wetu, Patrick Khanya ambaye ndiye mwenye shule hii, kwa kuwekeza rasilimali zake katika sekta ya elimu ambayo ndiyo msingi wa maendeleo ya nchi yetu.

“Shule yetu imekuwa ikipiga hatua mwaka hadi mwaka kitaaluma ikiwa na viwango vizuri vya ufaulu kwa wanafunzi wa kidato cha nne pamoja na michezo wanayofundishwa shuleni hapa."

“Shule inafundisha michezo soka, kikapu, pete, wavu na riadha, wapo watoto wengine wamepata ufadhili wa kujiendeleza kielimu na kimichezo nje ya nchi," amesema.

Amesema mwanafunzi mmoja alipata nafasi ya kujiendelea kimasomo na kimichezo nchini China, yeye anacheza mpira wa kikapu, wakati mwingine yuko nchini Hispania katika timu ya vijana wenye umri chini ya miaka 17 ya miaka ya soka duniani, Barcelona.

“Naomba nichukue fursa hii kuelezea kwa kifupi kuhusu maendeleo ya shule na changamoto zilizopo.

“Ndugu mgeni rasmi, shule hii ya Trust St.Patrick ni moja ya shule zilizopo ndani ya Jiji la Arusha inayofanya vizuri kitaaluma," amesema.

Mkuu wa Utawala wa shule hiyo, Dinnah Patrick, amesema kuwa, wao kazi yao kubwa ni kuhakikisha wanawawezesha watoto kujitambua na kutimiza ndoto zao.

"Tunawalea watoto hao katika maadili mema na wajitambue, lakini yote hayo bila nidhamu na malezi bora, hatuwezi kufanikiwa, ndiyo maana tupo nao karibu sana kuhakikisha wanatimiza ndoto zao," alisema.

Naye, mgeni rasmi, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Arusha, Suleiman Msumi amesema dhamira ya serikali ni kuona elimu inatolewa kwa kiwango bora na kila mhitimu anapata elimu bora itakayomwezesha kuendelea na kidato cha tano.

“Naipongeza shule kwa kutoa elimu kwa watoto wa kike kwa shule ya msingi na wavulani kwa upande wa sekondari."

Katika risala zilizowasilishwa hapo, pamoja na hotuba ya mkurugenzi, niwapongeze sana kwa kuendelea kubaki kwenye shule 10 bora mkoani Arusha na ikiwa katika shule 100 bora nchini.

Amesema serikali inatambua mchango mkubwa wa Trust St.Patrick katika michezo, ambapo imekuwa mhimili mkubwa kwa mkoa kwenye michuano ya Umoja wa Michezo na Taaluma kwa Shule za Msingi (UMITASHUMTA) na michuano ya Umoja wa Michezo kwa Shule za Sekondari Tanzania (UMISSETA), kuanzia ngazi ya wilaya, mkoa, kanda hadi taifa.

Kutokana na malezi bora kitaaluma na kimaadili, Mkurugenzi huyo aliuahidi uongozi wa shule hiyo kuwa, atashirikiana na wazazi na walezi wa wanafunzi wanaosoma shule maalum za mchepuo wa kingereza za serikali za mkoani humo kuwapeleka watoto wao shuleni hapo.

"Niwaahidi bodi ya shule pamoja na viongozi, nitawashawishi wazazi na walezi wa watoto waliokuwa wanasoma katika shule zetu za mchepuo wa kingereza za Enaboishu na Enyoreta kuwaleta watoto wao hapa Trust St. Patrick, naamini hawataniangusha," amesema.

Mbali na pongezi hizo, Mkurugenzi huyo aliushauri uongozi wa shule hiyo kuanzisha kidato cha tano kwani ina miundombinu yote inayotakiwa na wizara ya elimu.

Amesema litakuwa jambo la busara kama wataanza na wanafunzi wa kidato cha tano wasichana, huku akiamini kutokana na mazingira yalivyo, watafanya vizuri kitaaluma.

Naye, Meneja wa shule hiyo, Mike Patrick, amesema kuwa, wamewaandaa vizuri vijana wao ambao wataanza mitihani yao ya kumaliza kidato cha nne Novemba mwaka huu, huku darasa la awali na la saba wao tayari wamefanya mitihani yao.

Wanafunzi waliokuwa wakisherehekea kuhitimu ni kuanzia ngazi ya awali, darasa la saba na kidato cha nne.

 

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Arusha, Suleiman Msumi (katikati), Mkuu wa Utawala wa shule hiyo, Dinnah Patrick na Mkutugenzi wa Trust St.Patrick, Patrick Khanya.

Walimu na wafanyakazi wa shule za Trust St.Patrick ya jijini Arusha wakiwa kwenye picha ya pamoja

Wanafunzi wa kidato cha nne 2023

Wanafunzi wa kidato cha nne 2023

                                                 Wanafunzi wa darasa la saba 2023
Wanafunzi wa darasa la saba 2023

Wanafunzi wa darasa la awali 2023, wanaotarajiwa kuanza darasa la kwanza 2024
                             


                                                  Burudani mbalimbli zilitolewa na wanafunzi 
Moja ya majengo ya shule za Trust St.Patrick iliyopo jijini Arusha

No comments