Header Ads

ad

Breaking News

SIMBA YASONGA MBELE HATUA YA MAKUNDI LIGI YA MABINGWA AFRIKA


WAWAKILISHI wengine kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, Simba, imefanikiwa kusonga mbele kwenye michuano hiyo baada ya kunufaika na bao la ugenini dhidi ya Power Dynamo ya Zambia.

Katika mchezo wa pili uliopigwa Uwanja wa Chamazi jijini Dar es Salaam, wenyeji Simba walifungana bao 1-1 na wageni wao. Bao la kusawazisha la Simba lilifungwa na beki Kondwani Chiboni dakika ya 68, baada ya kujifunga akiwa katika harakati za kuokoa mpira.

Power Dynamo ilipata bao la kuongoza kupitia kwa Andy Boyeli dakika ya 16 , kwa shuti kali lililomshinda kudaka kipa wa Simba, Ayoub Lakred.

Kipindi cha pili Simba walikuwa wakiliandama lango la wapinzani wao na kusababisha  beki beki Kondwani Chiboni kuusukumiza mpira kimiani dakika ya 68, wakati akijaribu kuokoa mpira uliopigwa na John Bocco.

Kwa matokeo hayo, Simba wamesonga mbele hatua ya makundi kwa mabao ya ugenini, baada ya mechi ya kwanza iliyopigwa nchini Zambia kutoka sare ya mabao 2-2, na kuwa na jumla ya mabao 3-3.






No comments