Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Samia Suluhu Hassan akizungumza na Viongozi, Watumishi wa Sekta ya Afya pamoja na wageni mbalimbali kutoka ndani na Nje ya Nchi wakati akizindua Ripoti ya Utafiti wa afya ya Uzazi na mtoto na Viashiria vya malaria Tanzania kwa mwaka 2022 kwenye hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam, Oktoba 28,2023.

Msanii Mrisho Mpoto akitumbuiza wakati wa hafla ya uzinduzi wa Ripoti ya Utafiti wa afya ya Uzazi na mtoto na Viashiria vya malaria Tanzania kwa mwaka 2022 iliyofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.

Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Ummy Hamis Nderiananga akifurahia jambo wakati wa uzinduzi wa Ripoti ya Utafiti wa afya ya Uzazi na mtoto na Viashiria vya malaria Tanzania kwa mwaka 2022 iliyofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam Oktoba 28,2023.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Samia Suluhu Hassan akimkabidhi Kitabu Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Dkt. John Jingu mara baada ya uzinduzi wa Ripoti ya Utafiti wa afya ya Uzazi na mtoto na Viashiria vya malaria Tanzania kwa mwaka 2022 kwenye hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam  Oktoba 28, 2023.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan akimkabidhi Kitabu Balozi wa Marekani nchini Tanzania, Michael Battle mara baada ya uzinduzi wa Ripoti ya Utafiti wa afya ya Uzazi na mtoto na Viashiria vya malaria Tanzania kwa mwaka 2022 kwenye hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam, Oktoba  28, 2023.