MBUNGE UMMY AGAWA MAJIKO, MITUNGI YA GESI KWA MAMA LISHE 315 JIJINI TANGA
Mbunge wa Tanga Mjini, Ummy Mwalimu akionesha chupa ya soda aina ya Coca Cola, wakatio wa hafla ya kugawa majiko na mitungi ya gesi kwa kina Mama Lishe jimboni kwake Tanga mjini. |
Na Mwandishi Wetu, Tanga
MBUNGE wa Tanga Mjini, Ummy Mwalimu, leo Oktoba 15,2023 amegawa majiko ya gesi 80, mitungi mikubwa ya gesi ya kilo 15, 80, meza 80 na kreti za soda 80 kwa wajasiriamali wanawake wanaojihusisha na biashara ya chakula (Mama Lishe/Mama Ntilie) wa jijini Tanga. Jumla ya wanawake wajasiriamali 315 watanufaika na vifaa hivi.
Vifaa vilivyotolewa chini ya Kampeni ya Mwanamke Shujaa vimedhaminiwa na Kampuni ya Cocacola Kwanza na Oryx Gas Tanzani, kupitia kampeni yenye kauli mbiu ya Mwanamke Shujaa, Jiamini, Jithamini na Jijenge. Kampeni hii pia imeshirikisha Taasisi ya Ustawi wa Jamii, Korogwe FM na TK FM Radio ya Tanga.
Aidha, Ummy amewachangia katoni za soda 160, ambapo kila biashara ya Mama Lishe itapata katoni 2.
Ummy amewashukuru Coca Cola na Oryx kwa kuunga mkono jitihada zake Mbunge wa Tanga Mjini na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan za kuwawezesha wanawake kiuchumi. Aidha, Ummy amewashukuru kwa kukubali ombi lake la kuja Tanga awamu ya pili ili kuwapatia Mama Lishe vifaa hivyo muhimu vya mtaji ili kuwawezesha kiuchumi.
Akizungumza katika ghafla hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa Coca Cola, Unguu Sulay amesema kuwa, Kampuni ya Coca Cola itaendelea kuunga mkono jitihada za Rais Samia kwa kuwezesha wananchi kiuchumi hususani wanawake. Aidha, ameeleza kuvutiwa na kazi kubwa na nzuri ya Mbunge Ummy katika kuwatumikia watanzania na wananchi wa Tanga Mjini na ndiyo maana wameamua kumuunga mkono.
Hafla hiyo ya kukabidhi mitungi, majiko ya gesi, meza na kreti moja yenye soda, imehudhuriwa na Naibu Meya wa Jiji la Tanga, Rehema Mhina, Mkurugenzi Mkuu wa Coca Cola, Unguu Sulay, Kaimu Mkurugenzi Jiji la Tanga, Kizito, viongozi wa CCM na wajasiriamali wanawake wa Tanga Mjini.
No comments