Header Ads

ad

Breaking News

MATINYI AWATAKA WAKUU WA MIKOA, WAKURUGENZI KUELEZA MIRADI WANAYOTEKELEZA



Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Habari MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali, Mobhare Matinyi.

Na Mwandishi Wetu

MKURUGENZI wa Idara ya Habari MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali, Mobhare Matinyi, amesema Serikali inapeleka fedha nyingi kwenye halmashauri zote nchini, kwa lengo la utekelezaji wa miradi mbalimbali, lakini haitangazwi.

Akizungumza na wahariri na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Oktoba 29,2023, Matinyi amesema kuwa, fedha hizo zinafanya kazi ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa shule, maji, barabara ikiwemo afya, lakini taarifa za utekelezaji wa miradi hiyo watanzania wengi hawazipati.

Matinyi amekutana na wahariri na waandishi wa habari kwa mara ya kwanza  tangu ateuliwe na Rais Samia Suluhu Hassan kushika wadhifa huo, akichukua nafasi ya Gerson Msigwa ambaye ameteuliwa kuwa Katika Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo. Kabla ya uteuzi huo Matinyi alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Temeke.

Amesema Idara ya Habari Maelezo imepanga kuzindua prongramu maalumu ya taarifa za utekelezaji wa miradi ya maendeleo mikoani ifikapo Novemba Mosi mwaka huu mkoani Dodoma, ili kuwapa nafasi Wakuu wa mikoa na wakurugenzi wa halmashauri kuwaeleza watanzania mambo yanayofanywa na Serikali katika maeneo yao.

Matinyi amesema hatua hiyo itawapa nafasi wakuu wa mikoa na wakurugenzi kuelezea utekelezaji wa miradi katika maeneo yao, ukizingatia fedha hupelekwa katika halmashauri ambao,  utekelezaji wake hufanyika.

Amesema baada ya kuzindua Dodoma, watahamia mkoani Morogoro, Pwani na Dar es Salaam ambayo itakuwa ni awamu ya kwanza, mikoa ya Tanga, Kilimanjaro, Manyara na Arusha itakiuwa awamu ya pili.

Mkurugenzi huyo ameongeza kwamba, mambo mengi ya maendeleo  yanaendeshwa kwenye halmashauri, lakini hayajulikana,  akitaja fedha zinazojulikana kwa jina la asilimia 10 ya Mama, ambazo wengi hawazifahamu.

Amesema fedha hizo ambazo ni asilimia 10 ya mapato ya halmashauri, hutumika kwa kwa mgawanyo maaalumu wa asilimia nne kina mama, vijana asilimia 4 na asilimia mbili kwa watu wenye ulemavu, fedha ambazo ni mikopo zinazotakiwa kurejeshwa bila riba.

Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Deodatus Balile, amesema tangu kuingia madarakani kwa Serikali ya Awamu ya Sita, ushirikiano wa serikali n a vyiombo vya habari umeongezeka.

Amesema hatu hiyo imetokana na uongozi unaojua umuhimu wa vyombo vya habari, lakini tatizo lililopo hivi sasa lipo kwa baadhi ya mawaziri ambao hawatoi ushirikiano, ndiyo wanaolalamikiwa na vyiombo vya habari.

"Wapo mawaqziri hawatoi ushirikiano kabisas, hawa ndiyo wanaolalamikiwa na vyombo vya habari, tunakuomba malalamiko haya ya vyombo vya habari kwa mawaziri, utufikishie. Sisi tunataka ushirikiano utakaotuwezesha kupata taarifa sahihi," amesema.

Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Habari MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali, Mobhare Matinyi na Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Deodatus Balile





Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Deodatus Balile, akieleza jambo katika mkutano wa wahariri na Mkurugenzi Idara ya Habari MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali, Mobhare Matinyi


No comments