Header Ads

ad

Breaking News

Matembezi, upimaji wa magonjwa ya moyo ulivyofanyika

Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Temeke ambaye sasa ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari – MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali, Mobhare Matinyi akiongoza matembezi ya kuhamasisha jamii kufanya mazoezi na kupima afya ikiwa ni njia moja wapo ya kupambana na magonjwa yasiyoambukiza yakiwemo ya moyo. Matembezi hayo ya umbali wa kilometa nne yalifanyika hivi karibuni kuanzia  uwanja wa Uhuru hadi Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI), Hospitali ya Dar Group.

Wananchi waliopata huduma ya upimaji na matibabu ya moyo wakati wa maadhimisho ya siku ya moyo Duniani yaliyofanyika hivi karibuni katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) hospitali ya Dar Group wakipewa dawa za kutibu maradhi mbalimbali waliyokutwa nayo. Watu 604 walipata huduma za matibabu kati yao 99 walifanyiwa vipimo vya kuangalia jinsi moyo unavyofanya kazi na mfumo wa umeme wa moyo na 58 wanahitaji kupata matibabu ya kibingwa.

Kikundi cha Wasafi Jogging wakiwa katika  matembezi ya kuhamasisha jamii kufanya mazoezi na kupima afya ikiwa ni njia moja wapo ya kupambana na magonjwa yasiyoambukiza yakiwemo ya moyo. Matembezi hayo ya umbali wa kilometa nne yalifanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam kuanzia  uwanja wa Uhuru hadi Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) hospitali ya Dar Group.

Mkuu wa Kitengo cha Utafiti na Mafunzo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Pedro Pallangyo akitoa ushauri wa jinsi ya kutumia dawa za moyo  kwa mwananchi aliyefika  JKCI Hospitali ya Dar Group kwaajili ya kupata huduma ya upimaji na matibabu ya  moyo wakati wa maadhimisho ya siku ya moyo duniani. Watu 604 walipata huduma za matibabu kati yao 99 walifanyiwa vipimo vya kuangalia jinsi moyo unavyofanya kazi na mfumo wa umeme wa moyo na 58 wanahitaji  kupata matibabu ya kibingwa.

Askari wa Jeshi la Polisi wakiwa katika  matembezi ya kuhamasisha jamii kufanya mazoezi na kupima afya ikiwa ni njia moja wapo ya kupambana na magonjwa yasiyoambukiza yakiwemo ya moyo. Matembezi hayo ya umbali wa kilometa nne yalifanyika hivi karibuni kuanzia  uwanja wa Uhuru hadi Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) hospitali ya Dar Group.

Afisa Utafiti na Mafunzo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Saad Kamtoi akichukuwa taarifa za mwananchi aliyefika JKCI hospitali ya Dar Group kwaajili ya upimaji na matibabu ya moyo wakati wa maadhimisho ya siku ya moyo Duniani yaliyofanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam.

Afisa Lishe wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Husna Faraji akitoa elimu ya lishe bora kwa wananchi waliofika JKCI hospitali ya Dar Group kwaajili ya upimaji na matibabu ya moyo wakati wa maadhimisho ya siku ya moyo Duniani yaliyofanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam.


Wananchi waliopata huduma ya upimaji na matibabu ya moyo wakati wa maadhimisho ya siku ya moyo Duniani yaliyofanyika hivi karibuni katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) hospitali ya Dar Group wakipewa dawa za kutibu maradhi mbalimbali waliyokutwa nayo. Watu 604 walipata huduma za matibabu kati yao 99 walifanyiwa vipimo vya kuangalia jinsi moyo unavyofanya kazi na mfumo wa umeme wa moyo na 58 wanahitaji kupata matibabu ya kibingwa.

Rais wa Chama cha Madaktari Bingwa wa Moyo Tanzania (TCS) Robert Mvungi akisikiliza mwananchi aliyefika  JKCI Hospitali ya Dar Group kwaajili ya kupata huduma ya upimaji na matibabu ya  moyo wakati wa maadhimisho ya siku ya moyo duniani. Watu 604 walipata huduma za matibabu kati yao 99 walifanyiwa vipimo vya kuangalia jinsi moyo unavyofanya kazi na mfumo wa umeme wa moyo na 58 wanahitaji  kupata matibabu ya kibingwa.Picha zote na JKCI

No comments