Header Ads

ad

Breaking News

KAMATI YARIDHISHWA KASI YA MAENDELEO MSALALA

Mkurugenzi Mtendaji (W), Khamis Katimba akielezea namna alivyofanikiwa  kuziba mianya ya utoroshaji mapato ikiwemo ushirikishwaji watendaji kata, vijiji na wananchi katika kufichua watu wanaokwepa kulipa kodi pamoja na kutoa elimu kwa jamii.

Na Mwandishi Wetu

KAMATI ya Fedha, Uongozi na Mipango ya Halmashauri ya Msalala, Kahama imeeleza kuridhishwa na kasi ya maendeleo pia usimamizi wa miradi ndani ya halmashauri.

Wakizungumza katika kikao kilichoketi tarehe 23 Oktoba 2023, kwa ajili ya kupitia taarifa ya utekelezaji wa robo ya kwanza kwa Mwaka wa Fedha 2023/24, wajumbe hao walimpongeza mkurugenzi wa halmashauri hiyo, Khamis Katimba kwa kusimamia na kutekeleza miradi hiyo vizuri na ndani ya muda.

Diwani wa Kata ya Segese, Joseph Manyara alisema, madiwani waliweka malengo mengi baada ya mkurugeni Katimba kuanza kazi katika halmashauri hitio ana na kwamba, vingi vimefikiwa kabla ya muda.

“Pamoja na malengo mengine yaliyofikiwa, tulitaka Ofisi za Halmashauri ya Msalala zinahamie kwenye majengo yake ndani ya miezi sita, lakini ametekeleza hilo ndani ya miezi minne baada ya kuteuliwa.

Diwani hiyo, pia alipongeza watangulizi wa mkurugeni huyo ambapo ni Simon Berege Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Shinyanga Vijijini na Charles Fussi, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mufindi kwa kuacha mazingira mazuri yaliyomsaidia Katimba kufikia malengo

Diwani wa Kata ya Ikinda, Matrida Msoma alisema, Katimba kafanikiwa kuvusha kiwango cha makusanyo ya yedha katika robo ya kwanza ya Mwaka wa Fedha 2023/24.

“Kigezo kingine kilichotumika kupima utendaji wa ndugu Khamis Katimba ni suala zima la ukusanyaji mapato ambapo hadi kufikia Septemba 30, 2023, halmashauri imewezeshwa kukusanya Tsh. 3,795,485,236.34 sawa na 37% ya lengo la kukusanya 5,700,000,000.00 huku matumizi yakiwa ni Tsh. 2,765,856,143.28 sawa na 23% ya matumizi kwa mwaka 2023-24,” alisema Mosma.

Akisoma taarifa ya fedha kwenye kikao hicho, Mweka Hazina wa halmashauri hiyo, Gordon Dinda alisema, katika robo hii, shughuli nyingi za maendeleo zimefanyika ikiwemo ujenzi wa shule mpya ya msingi Kabale yenye madarasa 12, maktaba na matundu ya vyoo 10.

Dinda alisema, Serikali ilitoa fedha kupitia mradi wa Boost ambapo jumla ya Tsh. 561,000,000.00 zilitumika huku wananchi wakitumia nguvu zao katika ukusanyaji wa mawe na mchanga.

“Kwenye shule hiyo ya Kabale, kuna madarasa manane yamejengwa, jengo la utawala, Maabara tatu, Jengo la Maktaba na Jengo la TEHAMA ambapo hadi kufikia Novemba 10, mradi utakamilika na jumla ya Tsh. 603,000,000.00 fedha za Serikali Kuu kupitia mradi wa SEQUIP zitatumika,” alisema. 

Alisema, miradi hii yote ipo katika Kata ya Bulyanhulu kwa kuwa, kata hiyo ina idadi kubwa ya wakazi kutokana na uwepo wa shughuli za uchimbaji madini.

“Kutokana na hiyo, halmashauri iliona ni vema kuongeza idadi ya shule pia kujenga Chuo cha Veta kupitia fedha zitolewazo na mgodi wa Bulyanhulu, lengo ni kuwezesha vijana wanaohitimu masomo katika shule hizo, kujengewa uwezo wa kujiajiri na kuajiriwa kupitia taaluma walizopata kutoka VETA,” alisema.

Madaiwani pia alipongeza hatua ya Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan, kuendelea kuthamini wananchi wa Msalala kwani ndio inaongoza kwa kupata fedha kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali.

Baadhi ya miradi hiyo ni ujenzi wa Hospitali ya Halmashauri ya Msalala, ujenzi wa vituo vine vya afya katika Kata za Segese, Mwalugulu, Isaka na Bulige, ujenzi wa shule mpya mbili ya Msingi na Sekondari katika Kata ya bulyanhulu.

Pia ujenzi wa stendi mpya mbili za Segese na Isaka ambapo mradi mkubwa zaidi, ni kuanza kwa matengenezo ya Barabara ya Kahama Kakola kwa kiwango cha lami ambapo inatazamiwa kuanza mwanzoni mwa Novemba 2023 kutokana na taarifa ya TANROAD, Mkoa wa Shinyanga.

Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Msalala, Flora Sagasaga ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Mwalugulu akichangia hoja katika kikao cha Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango akiwa na Mkurugenzi Mtendaji (W), Khamis Katimba.






No comments