EWURA YAVIFUNGIA VITUO VIWILI VYA MAFUTA
MAMLAKA ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), imevifungia vituo viwili vya mafuta kwa muda wa miezi sita kwa kosa la kuhodhi mafuta ili kujipatia maslahi haramu ya biashara, ikiwemo faida kubwa kutokana na ongezeko la bei za mafuta.
Mpango huo ni kinyume na sheria, kanuni na miongozo inayosimamia biashara ya mafuta nchini.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Oktoba 27, 2023 jijini Dar es Salaam, Meneja wa Mawasiliano na Uhusiano EWURA, Titus Kaguo, amesema vituo vilivyofungiwa ni GAPCO Tanzania Limited Moshi Service Station chenye namba ya leseni PRL – 2023 – 104 kilichopo Moshi Kilimanjaro.
Kaguo amekitaja Kituo kingine ni Anwar Saleh Bakhamis T/A Serious Oil Petrol Station chenye usajili wa leseni PRL – 2019 -228.
Amesema kuwa, vituo hivyo wamefanya kasa la kufunga vituo vya kuuza mafuta wakiwa bado wanamafuta jambo ambalo ni wamekiuka masharti ya uuza wa mafuta.
Kaguo amesema kuwa mpaka sasa jumla wamevifungia vituo vya kuuza mafuta 11 kwa kosa la kwa kosa la kuhodhi mafuta ili kujipatia maslahi haramu ya biashara ikiwemo faida kubwa kutokaba na ongezeko la bei za mafuta jambo ambalo ni kinyume na sheria, kanuni na miongozo inayosimamia biashara ya mafuta nchini.
“EWURA inapenda kuwakumbusha wafanyabiashara ya mafuta nchini kuhakikisha wanaendesha biashara zao kwa mujibu wa sheria, kanuni, na miongozo inayosimamia biashara ya mafuta nchini” amesema Kaguo.
Kwa mujibu wa Sheria ya Petroli, sura Na 392 EWURA ina jukumu la kuhakikisha upatikanaji wa mafuta wakati wote katika maeneo yote nchini.
Kuanzia mwezi Julai mwaka huu kumekuwepo na matukio kwa baadhi ya maeneo hasa pembeni mwa nchi kukosa mafuta hasa kipindi bei zinapoelekea kubadilishwa na kusababisha kuwa na usumbufu makubwa kwa wananchi na madhara ya kiuchumi.
"Kuanzia Julai mwaka huu, maeneo ya pembeni wakati wa kuelekea kubadilishwa kwa bei, husababisha usumbufu mkubwa kwa wananchi na madhara ya kiuchumi," amesema.
Ili kufikia malengo EWURA inaendelea kuchukua hatua mbalimbali za kisheria ikiwemo kuvifungia baadhi ya vituo vilivyothibitika kufichua mafuta kinyume na kanuni na miongozo inayosimamia biashara ya mafuta nchini.
No comments