DKT.TULIA ACHAGULIWA KUWA RAIS WA MABUNGE DUNIANI
SPIKA wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson, amechaguliwa kuwa Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), katika uchaguzi uliofanyika Ijumaa Oktoba 27, 2023 jijini Luanda nchini Angola.
Dkt. Tulia ameshinda urais huo baada ya kupata kura 172 kati ya kura 303 zilizopigwa na anarithi mikoba ya Rais aliyemaliza muda wake, Duarte Pacheco kutoka Ureno.
Wagombea wengine walioshiriki katika uchaguzi huo ni Catherine Hara kutoka Malawi kura 61, Adji Diarra kutoka Senegal kura 51 na Marwa Hagi kutoka Somalia kura 11.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Rais mteule wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) Mhe. Dkt. Tulia Ackson, akiwashukuru aajumbe waliompigia kura na kushinda nafasi hiyo Oktoba 27, 2023 jijini Luanda, Angola. Dtk. Tulia ameshinda kwa kupata kura 172 kati ya 303. PICHA NA OFISI YA BUNGE
No comments