KAMATI YA BUNGE YAIPONGEZI BMT KUENDELEZA MICHEZO
Na Shamimu Nyaki.
KAMATI ya Bunge ya Elimu, Utamaduni na Michezo chini ya Mwenyekiti, Husna Sekiboko imelipongeza Baraza la Michezo la Taifa kwa kuendelea kusimamia Sekta ya michezo ambayo kwa sasa inaitangaza vyema Tanzania na kusimamia Utawala Bora ambao umepunguza migogoro katika Sekta hiyo.
Pongezi hizo zimetolewa baada ya kuwasilishwa kwa Taarifa ya Utekekezaji wa Majukumu ya Baraza hilo leo Oktoba 25, 2023 jijini Dodoma, iliyowasilishwa na Neema Msitha kwa niaba ya Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Damas Ndumbaro.
Akiwasilisha taarifa hiyo, Msitha amesema sekta hiyo imeendelea kupata mafanikio makubwa ikiwemo kuwa mwenyeji wa mashindano ya AFCON mwaka 2027, kuanzishwa kwa Mfuko wa Maendeleo ya Michezo ambao umesaidia timu za Taifa katika mashindano mbalimbali.
BMT imefanikiwa kuanzisha mfumo wa Kidigitali, Usajili wa Vyama na Mashirikisho, na Michezo mbalimbali ikiwemo Riadha, timu za mpira wa miguu, netiboli, gofu, ngumi zimefaidika na Mfuko wa Maendeleo ya Michezo,” amesisitiza Msitha.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa kamati, Husna Sekiboko ameielekeza Wizara iangalie namna bora ya kusimiamia vyema idara zinazosimamia Maendeleo ya Michezo ngazi ya mikoa na halmashauri na kuhakikisha mtiririko wa asilimia tano za michezo ya kubahatisha inafika kwa wakati.
Wakichangia taarifa hiyo, wajumbe wa kamati hiyo wamepongeza uhusiano uliopo kati ya Wizara inayosimamia michezo Tanzania Bara na Zanzibar, huku wakishauri kuajiri walimu wa michezo, kufanyika mashindano mbalimbali ikiwemo Taifa Cup na kuhakikisha asilimia tano ya michezo ya kubahatisha inafanya kazi yake ipasavyo.
No comments