Yanga ya moto, yaipasua Al-Merrikh 2-0
MABINGWA wa Ligi Kuu Tanzania Bara na washindi wa pili wa Kombe la Shirikisho Barani Afrika, Yanga, wameendeleza furaha kwa wana Jangwani na Watanzania baada ya kuigaragaza Al-Merrikh mabao 2-0, katika mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa Pele Kigali nchini Rwanda.
Katika mchezo huo, Yanga ilipata bao la kwanza kupitia kwa dakika ya 60, lililofungwa na Kennedy Musonda kwa kichwa akiunganisha mpira wa adhabu uliopigwa na Pacome Zouzoua.
Bao la pili lililowamaliza nguvu Al-Merrikh liliwekwa kimiana na mshambulizi kinda wa Yanga, Clement Mzize dakika ya 78, akitumia vizuri pasi ya kisigino iliyopigwa na Stephane Aziz K.
Yanga imeonesha ubora wake katika mchezo huo, ikiwa kama ni mwendelezo wa msimu uliopita kwenye mechi za Kombe la Shirikisho, ambako ilitinga fainali.
Kwa matokeo hayo, Yanga imejiweka katika nafasi nzuri ya kusonga mbele kwenye michuano hiyo ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika.
No comments