Header Ads

ad

Breaking News

VIFURUSHI VINAWEZESHA WATOTO NA WAZAZI WAO KUJIUNGA - NHIF

                                                             
Na Mwandishi Wetu

WANANCHI wamehamasishwa kujiunga na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), kupitia mpango wa vifurushi unaowezesha watoto kujiunga na wazazi wao na kuwa na uhakika wa kupata huduma za matibabu.

Rai hiyo imetolewa na Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Afya na Masuala ya Ukimwi, wakati wajumbe wa Kamati hiyo walipotembea NHIF kwa lengo la kujifunza na kupata taarifa ya utekelezaji.

Akiwasilisha taarifa, Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Bernard Konga alisema kwa sasa watoto wanaweza kujiunga kupitia vifurushi wakiwa na wazazi wao.

"Tulipofanya maboresho ya usajili kwenye eneo la watoto tulifahamu kundi hilo ni la muhimu na ndiyo maana tulihakikisha tunaweka dirisha la kuwezesha watoto kujiunga na wazazi wao hivyo, nawaomba sana wazazi watumie fursa hii," alisema Konga.

Akichangia suala hilo, Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Dkt.Faustine Ndugulile, aliitaka NHIF kuwekeza kwenye utoaji wa elimu ili wananchi waone umuhimu na faida za kujiunga kupitia mpango huo.

"Wananchi wahamasishwe na wapewe elimu ya dhana ya Bima ya Afya kwamba, wanapojiunga kwa wingi ndiyo kunakuwa na ubimilivu wa Mfuko," alisema.

Kwa upande wa wajumbe wa Kamati hiyo, wameupongeza Mfuko kwa jitihada kubwa unazozifanya katika kutoa elimu na kulinda uhai wa Mfuko.

No comments