Header Ads

ad

Breaking News

Upatikanaji bidhaa za afya umefika asilimia 64- Mkurugenzi Mtendaji MSD

Mkurugenzi Mtendaji wa Bohari ya Dawa (MSD), Mavere Tukai, akizungumza na wahariri na waandishi wa habari leo Septemba 27,2023 jijini Dar es Saslaam

Na Frank Balile

BOHARI ya Dawa (MSD), imepata mafanikio katika sekta ya afya baada ya upatikanaji wa bidhaa za afya kuongezeka kutoka asilimia 51 kwa mwaka 2022 hadi kufikia asilimia 64 kwa mwaka 2023.

Akizungumza katika mkutano uliowakutana MSD na Wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari na kuratibiwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina leo Septemba 27,2023, jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa MSD, Mavere Tukai, amesema upatikanaji wa dawa umefikia asilimia 81, kwa Juni 2023 kutoka asilimia 57, Juni 2022.

Bohari ya Dawa (MSD), ni Taasisi ya Serikali iliyo chini ya Wizara ya Afya, iliyoanzishwa mwaka 1993 kwa mujibu wa Sheria ya Bohari ya Dawa iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2021.

Tukai amesema wamefanikiwa kupokea shilingi bilioni 190.3 kwa mwaka wa fedha 2022/23, ikilinganishwa na sh.bilioni 134.9 mwaka wa fedha wa 2021/22, ikiwa sawa na asilimia 95.

Mkurugenzi Mtendaji huyo amesema, mafanikio hayo yametokana na ushirikiano waliokuwa nao ndani ya taasisi na nje ya taasisi.

Wahariri wakifuatilia maelezo ya Mkurugenzi Mtendaji wa MSD, Mavere Tukai (hayupo pichani).

Amesema mapato kwa Agosti 2023, yameongezeka baada ya kupatikana shilingi bilioni 35.68, wakatihuku hali ya utendaji halisi shilingi bilioni 34.08.

Ameongeza kuwa, wametekelezaji wa mradi wa ununuzi na usambazaji wa vifaa vya huduma kwa wajawazito wanaopata uzazi pingamizi wakati wa kujifungua.

Amesema vipo vituo vya kutolea huduma vinavyopelekewa vifaa, ambapo jumla ya vifaa vilivyopangwa kusambazwa ni 345, lakini idadi ya vifaa vilivyosambazwa hadi kufikia Juni 2023 ni 299 sawa na asilimia 87.

Tukai ameobgeza kuwa, gharama za mradi wa thamani ya vifaa vinavyotarajia kusambazwa ni sh.bilioni 99.7, thamani ya vifaa vilivyosambazwa ni sh. bilioni 79.4, sawa na asilimia 80 za utekelezaji.

MKurugenzi Mtendaji huyo amesema taasi hiyo imeanzisha kitengo maalumu cha usimamizi na ufuatiliaji wa mikataba, huku ununuzi wa bidhaa za afya kutoka kwa wazalishaji wa ndani ukiongezeka kutoka shilingi bilioni 14.1 mwaka wa fedha 2021/22 hadi kufikia shilingi bilioni 39.77.

Amesema kuwa wameongeza idadi ya mikataba ya muda mrefu kutoka mikataba 100 yenye bidhaa za afya 711 kwa mwaka wa fedha 2021/22 hadi kufikia mikataba 233 yenye bidhaa 2,209 kwa mwaka wa fedha 2022/23.

Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano Ofisi ya Msajili wa Hazina, Erick Anthony Mkuti (kushoto), akiteta jambo na Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Deodatus Balile, wakati wa kikao kazi 

Kuhusu ujenzi wa wa Kiwanda cha mipira ya mikono 'gloves', kilichopo Idofi mkoani Njombe, Mkurugenzi huyo amesema umekamilika na kwamba wanaendelea kutambua sekta binafsi kwa maeneo ya uwekezaji ya bidhaa za afya za kimkakati za vidonge (tablets), rangi mbili (capsules), vimiminika na bidhaa zitokanazo na zao la pamba na kutangaza ushirikiano kati ya MSD na sekta binafsi.

Amesema wataanzishaji Kampuni Tanzu ya MSD Medipharma Manufacturing Company Ltd,  itakayosimamia uzalishaji wa bidhaa za afya na kwamba, wameboresha ushirikiano na kuongeza ushawishi katika ngazi ya SADC kupitia balozi zetu.

Mkurugenzi Mtendaji huyo amesema wameimarisha mifumo ya usimamizi kwenye ununuzi na usambazaji wa bidhaa za afya, ushirikiano na wadau wa mnyororo wa ugavi, kushirikisha balozi zetu zilizopo China, Algeria, Urusi na Korea ya Kusini kutafuta wadau wa uzalishaji na ununuzi.

Kwa upande wa TEHAMA, Tukai ameswema wameboresha mifumo simamizi kama usimamizi wa magari, kuanzisha kampuni tanzu ili kuweza kusimamia shughuli za uzalishaji wa bidhaa za afya kwa ufanisi, Ugatuzi wa utendaji kutoka makao makuu kwenda Ofisi za Kanda.

Tukai amesema pia wana mpango wa Kuanzisha  na kusimamia viwanda vya bidhaa za afya kwa kushirikiana na Sekta binafsi, Kuimarisha uhifadhi wa bidhaa za afya kwa kujenga maghala ya kisasa mikoa ya Kagera, Dar es Salaam na Mwanza.

Kusimika na kuimarisha matumizi ya TEHAMA kwenye kazi zote za taasisi, Kuimarisha matumizi ya takwimu kwenye kazi, Kuimarisha mfumo wa usimamizi wa watendaji wa taasisi, Kuongeza ushirikiano na wazalishaji wa ndani ili kuboresha upatikanaji wa bidhaa za afya.

Mkurugenzi Mtendaji huyo amesema wameboresha muundo wa taasisi kwa lengo la kuimarisha utendaji wa taasisi, ugatuzi wa shughuli zilizokuwa zikifanyika makao makuu kwenda Ofisi za Kanda na Kutumia vyanzo mbadala vya fedha ili kuongezea uwezo wa kifedha taasisi.

Wahariri wakisikiliza kwa makini

Meneja Uhusiano Bohari ya Dawa (MSD), Eti Kusiluka, akizungumza kwenye kikao kazi kati ya MSD na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari

Mhariri Mgaya Kingoba akiuliza swali katika kikao kazi kati ya wahariri na maafisi wa MSD kilichofanyika leo Septemba 27,2023 jijini Dar es Salaam

Afisa Uhusiano Mwandamizi Ofisi ya Msajili wa Hazina, Sabato Kosuri, akitoa mwongozo wa kikao hicho.

Maafisa wa MSD wakifuatilia maelezo ya Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi hiyo

Mkuurgenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD), Mavere Tukai (kushoto) na Mkuu wa Kitengo cha Habafri na Mawasiliano Ofisi ya Msajili wa Hazina, Erick Anthony Mkuti.

Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Mavere Tukai (katikati), akibadilishana mawazo na Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano Ofisi ya Msajili wa Hazina, Erick Anthony Mkuti na Meneja Mipango, Ufuatiliaji na Tathmini, Hassan Ali (kushoto).

Wahariri wakisikiliza kwa makini
Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD), Mavere Tukai (kushoto), akibadilishana mawazo na Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano Ofisi ya Msajili wa Hazina, Erick Anthony Mkuti (katikati) na Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Deodatus Balile katika mkutano wa wahariri na maafisa wa MSD.

No comments