Header Ads

ad

Breaking News

TUTAWADHIBITI WANAOWAONEA WANYONGE-RIDHIWANI KIKWETE

Na Mwandishi Wetu, Mara

NAIBU Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais anayeshughulikia Menejiment ya Utumishi wa Umma na Utawala ambaye pia ni Mbunge wa Chalinze,  ameanza ziara ya Mkoa wa Mara kwa kuzungumza na Watumishi wa Manispaa ya Musoma na kukagua utekelezaji wa mpango wa kuondoa Umaskini yaani TASAF katika mji huo. 

Ridhiwani ambaye ana ziara ya siku tatu katika Mkoa huo, aliwaelekeza Watumishi wa umma kujikita katika kuhakikisha wanazingatia na kutafsiri maono ya Rais Samia Suluhu Hassan.

Aliwahimiza kuwe na utumishi wenye kuleta tija, ubora ulio kimkakati unaolenga kuwatumikia Wateja ambao ni wananchi. 

Naibu Waziri aliwaasa kuwa watumishi wabunifu na wenye mikakati ili kufikia malengo.

Pia, katika tukio lingine, Naibu waziri Ridhiwani amewaondoa kwenye uratibu wa mpango wa TASAF waratibu wa Mkoa na Wilaya kwa kile alichokiita kushindwa kufikia malengo ya kuwahudumia wananchi wanyonge ambao wanahitaji huduma hiyo katika muda sahihi.

Akionesha kukasirishwa kwa kushindwa kutimiza wajibu wao, Ridhiwani alimweleza Katibu Tawala Mkoa wa Mara, Msalika Robert Makungu kutoelewa kwa nini hadi leo wahitaji hao hawajalipwa wakati fedha kwa ajili ya wanufaika zilitumwa ili walipwe wanufaika. 

Naibu Waziri anaendelea na ziara mkoani hapo kwa kuelekea Wilayani Tarime.





No comments