TANZANIA, MOROCCO KUSHIRIKIANA KATIKA MICHEZO
WAZIRI wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Morocco hapa nchini Mhe. Zakaria El Goumiri kuhusu ushirikiano baina ya Tanzania na Morocco katika Sekta ya Michezo.
Kikao hicho kimefanyika Septemba 13, 2023 katika ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar es Salam ambapo Waziri Mhe. Dkt. Ndumbaro amewasilisha salamu za pole kwa nchi hiyo kufuatia Tetemeko la Ardhi lililopita katika nchi hiyo. Na kumhakikisha Balozi huyo kuwa, Tanzania itaendelea kuimarisha ushirikiano baina ya nchi hizo mbili.
Kwa upande wake Balozi Mhe. Zakaria El Goumiri amepokea salamu za pole kutoka Tanzania, ambapo pia amesema nchi yake itaiunga mkono Tanzania katika ujenzi wa miondombinu ya michezo ili kuendelea kukuza vipaji vya wanamichezo ambao watakuwa ni hazina kwa mataifa hayo kwenye timu za taifa.
No comments