Header Ads

ad

Breaking News

Tanzania, Kenya, Uganda wenyeji wa AFCON 2027




Na Mwandishi Wetu

AFRIKA Mashariki, nchi za Tanzania Kenya na Uganda kwa pamoja wataandaa mashindano ya Mataifa ya Afrika (AFCON), yaliyopangwa kufanyika 2027.

Katika kinyang'anyiro cha kuwania kuandaa, nchi za Afrika Mashariki zilifanikiwa kuziangusha nchi nyingine na kupata nafasi ya kuandaa mwaka 2027, wakati Morocco wao wataandaa mashindano ya mwaka 2025.

Mashindano hayo mwaka huu 2023 yalitakiwa kufanyika, lakini alisogezwa mbele hadi Januri 13, 2024 nchini Ivory Coast.

AFCON ya mwaka 2021 ilifanyika nchini Cameroon, ambapo Senegal ilibeba ubingwa kwa kuwafunga Misri kwa mikwaju ya penalti 4-2.

Kutoka kanda kubwa ya Afrika Mashariki, Sudan na Ethiopia pekee ndizo zilizoweza kuandaa mashindano haya.

Sudan iliandaa mashindano ya kwanza ya AFCON mwaka 1957 na tena mwaka 1970. Ethiopia iliandaa mashindano ya mwaka 1962 na 1976.

No comments