Header Ads

ad

Breaking News

Simba, Power Dynamos zatosa sare 2-2



Na Mwandishi Wetu, Ndola

TIMU ya soka ya Simba, imewabana wenyeji Power Dynamos ya Zambia katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika iliyopigwa kwenye Uwanja wa Levy Mwanawasa mjini Ndola nchini Zambia.

Katika mchezo huo, kiungo fundi wa timu hiyo, Clatous Chota Chama, ndiye aliyewanyima ndugu zake ushindi baada ya kuifungia timu yake mabao yote mawili na kuiwezesha kutoka sare ya mabao 2-2.

Simba watahitaji sare ya bao au ushindi wowote kwenye mchezo huo utakaochezwa Uwanja wa Azam Complex jijini Dar es Salaam.





No comments