Header Ads

ad

Breaking News

RAIS DKT.MWINYI KUSHIRIKI MKUTANO WA G77+CHINA NCHINI CUBA


Na Mwandishi Wetu

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,DkT. Hussein Ali Mwinyi ameondoka Zanzibar kuelekea Havana, Cuba kumwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Samia Suluhu Hassan, katika Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Kundi la 77 na China (G77+ China) utakaofanyika tarehe 15 hadi 16 Septemba 2023.

Mkutano huo unalenga kukutanisha mataifa yanayoendelea ili kujadili changamoto zinazoikabili dunia, hasa baada ya kuathirika na UVIKO-19, migogoro inayoendelea duniani na vikwazo mbalimbali vya kiuchumi.  

Mkutano huo utajikita zaidi katika kutafuta njia bora ya kujenga ustahimilivu kupitia maendeleo ya sayansi na teknolojia na ubunifu ili kundi la G77 na China liweze kufikia malengo yake kwa pamoja.

Mkutano huo utaongozwa na kaulimbiu isemayo Current Development Challenges: The Role of Science, Technology and Innovation.

Rais Dkt.Mwinyi anatarajiwa kuhutubia mkutano huo na kuelezea vipaumbele vya Tanzania, pamoja na hatua zilizochukuliwa kukuza tafiti na kuimarisha matumizi ya sayansi, teknolojia na ubunifu (STI) katika kuleta mapinduzi ya kiuchumi. 



No comments