NSSF YAELEZEA MAFANIKIO YAKE
![]() |
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Masha Mshomba akizungumza na wahariri wa vyombo vya habari (hawapo pichani), jijini Dar es Salaam Septemba 25,2023 |
Na Mwandishi Wetu
MFUKO wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) ,umesema umepata mafanikio makubwa, baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Samia Suluhu Hassan kuweka mazingira mazuri yaliyowasaidia kusajili wanachama wengi na kuongeza mchango wa mfuko huo na kufikia sh. trilioni 1.7 katika hesabu zake ambazo zinakaguzliwa na Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).
Kati ya Machi Mosi, 2021 na Juni 30, 2023, waliandikisha jumla ya wanachama 547,882, ambapo idadi ya wanachama wachangiaji iliongezeka kwa asilimia 36.
Ni kutoka 874,082 Machi Mosi, 2021 hadi kufikia wanachama 1,189,222 Juni 30, 2023 ikichangiwa na mkakati wa Serikali wa kuvutia wawekezaji, pamoja na utekelezaji wa mpango wa mfuko katika uandikishaji wanachama.
![]() |
Wakurugenzi wa Idara mbalimbali wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), wakisikiliza majadiliano |
Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Masha Mshomba, ameyazungumza hayo leo Septemba 25, 2023, katika kikao kazi na wahariri wa vyombo vya habari nchini, inayoratibiwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina.
Amesema taasisi ya 16, kati ya taasisi na mashirika yaliyo chini ya Msajili wa Ofisi ya Hazina, ambapo Msajili wa Hazina, Nehemiah Mchechu, ameyaelekeza kukutana na wahariri ili kueleza umma yalipotoka, yalipo, yanapoelekea na mafanikio yake.
NSSF ulianzishwa mwaka 1964, kama kitengo ndani ya Wizara ya Kazi kinachoshughulikia mafao ya wafanyakazi baada ya kustaafu, ambapo mwaka 1975, kitengo hicho kiliboreshwa na kuwa taasisi inayojitegemea iliyoitwa National Provident Fund (NPF).
![]() |
Wahariri wa vyombo vya habari wakisikiliza |
Maboresho zaidi yalifanyika mwaka 1997, wakati Sheria Na. 28 ilitungwa na kuibadili NPF kuwa Mfuko wa Pensheni, hivyo kuwezesha kuwa na wigo mpana wa kutoa huduma za hifadhi ya jamii kwa wafanyakazi.
Mwaka 2018 Serikali ilifanya maboresho ya Sekta ya Hifadhi ya Jamii yaliyosababisha kurekebishwa kwa Sheria ya Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii, (The National Social Security Fund) Sura ya 50.
Uamuzi huo uliifanya NSSF kuwa mfuko pekee unaohudumia hifadhi ya jamii kwa wafanyakazi wa sekta binafsi na wale wa sekta isiyo rasmi nchini.
Mshomba amesema wanachama wachangiaji katika mfuko wameongezeka kwa asilimia 26 hadi kufikia wanachama wachangiaji 1,189,222, Juni 30,2023 ikilinganishwa na wanachama wachangiaji 945,029 waliofikiwa Juni 30, 2021.
Mkurugenzi Mkuu huyo amesema katika mwaka wa fedha ulioishia Juni 30, 2023, makusanyo ya michango kwa mwezi iliongezeka kutoka shilingi bilioni 97.67 iliyofikiwa Machi Mosi, 2021 hadi kufikia shilingi bilioni 143.05 kwa mwezi katika mwaka wa fedha ulioishia Juni 30,2023.
“Ongezeko hili limechangiwa na kuongezeka kwa waajiri wanaoleta michango kwa wakati na mazingira mazuri ya ufanyaji biashara kwa sekta binafsi.”
Mshomba amesema makusanyo ya michango kwa mwaka yameongezeka kwa asilimia 43 hadi kufikia shilingi bilioni 1,718.28 katika mwaka ulioishia Juni 30,2023 ukilinganisha na shilingi bilioni 1,201.05 zilizokusanywa katika mwaka ulioishia Juni 30,2021.
“Uwekezaji wa Mfuko uliongezeka kwa asilimia 111 kutoka shilingi bilioni 3,395.46 tarehe 1 Machi 2021 hadi kufikia shilingi bilioni 7,153.23, Juni 30, 2023 ikichangiwa na kukua kwa thamani ya vitega uchumi, michango ya wanachama na mapato ya uwekezaji.”
![]() |
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Masha Mshomba (kushoto), akijadiliana jambo na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Ofisi ya Msajili wa Hazina, Erick Anthony Mkuti. |
Pia, amesema thamani ya vitega uchumi vya mfuko imekua kwa asilimia 55 hadi kufikia shilingi bilioni 7,153.23, Juni 30, 2023 kutoka shilingi bilioni 4,622.25 zilizofikiwa Juni 30, 2021.
Mkurugenzi huyo ameweka wazi kuwa, wastani wa mapato ya uwekezaji kwa mwezi katika mwaka wa fedha ulioishia Juni 30, 2023, yalifika shilingi bilioni 72.06 ikiwa ni ongezeko la asilimia 92 ukilinganisha na shilingi bilioni 37.35 zilizokusanywa Machi 2021.
Amesema mapato halisi ya mfuko yameongezeka kutoka wastani wa asilimia 3.31, Machi 2021 hadi kufikia asilimia 5.32 katika kipindi kilichoishia Juni 30, 2023.
![]() |
Mkuu wa Kitengo cha Habari Ofisi ya Msajili wa Hazina, Erick Athony Mkuti (kushoto), akiteta jambo na Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Deodatus Balile |
“Mapato ya uwekezaji kwa mwaka yameongezeka kwa asilimia 93 na kufikia shilingi bilioni 864.76 katika mwaka wa fedha ulioishia Juni 30, 2023 ukilinganisha na shilingi bilioni 448.17 zilizokusanywa katika mwaka wa fedha Juni 30, 2021.”
Mkurugenzi Mkuu huyo amesema katika mwaka wa fedha ulioishia Juni 30, 2023, mfuko ulilipa shilingi bilioni 61.93 kwa mwezi kama mafao kwa wanufaika mbalimbali ikiwa ni ongezeko la asilimia 22 ukilinganisha na shilingi bilioni 50.58 zilizolipwa kwa mwezi kipindi kilichoishia Machi Mosi, 2021.
Mshomba amesema, malipo ya mwaka ya mafao kwa wanufaika mbalimbali wa mfuko yaliongezeka kwa asilimia 25 na kufikia shilingi bilioni 743.17 katika mwaka wa fedha ulioishia Juni 30, 2023 ukilinganisha na shilingi bilioni 594.33 zilizolipwa katika mwaka wa fedha ulioshia Juni 30, 2021.
![]() | |
|
![]() |
Mhariri Bakari Kimwanga, akiuliza swali katika mkuutano huo |
![]() |
Meneja Uhusiano wa NSSF, Lulu Mengele, akizungumza katika mkutano wa wahariri na uongozi wa NSSF unaoratibiwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina jijini Dar es Salaam leo Septemba 25,2023. |
![]() |
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Masha Mshomba akizungumza na wahariri wa vyombo vya habari (hawapo pichani), jijini Dar es Salaam Septemba 25,2023 |
No comments