Header Ads

ad

Breaking News

Mihanji ampongeza Mafuru kwa mageuzi makubwa AICC, JNICC

Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Jane Mihanji akitoa neno la shukrani

Na Frank Balile

MJUMBE wa Kamati ya Utendaji ya Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Jane Mihanji, amempongeza Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Arusha (AICC), Ephraim Mafuru kwa kufanya mageuzi makubwa katika taasisi hiyo.

Mihanji, ambaye pia ni mhariri wa magazeti ya Uhuru na Mzalendo, amesema AICC na Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC), tangu waanze mageuzi makubwa ikiwemo ajira kwa watendaji vijana wenye uwezo, wamefanikiwa  kutimiza malengo yao.

Amewataka viongozi wa taasisi hiyo kuhakikisha wanatimiza malengo yao waliyojiwekewa kwa mwaka 2023/2024 la kukusanya zaidi ya shilingi bilioni 120, huku akisisitiza ushirikiano waliouanzisha wauendeleze.

Naye, Mkurugenzi Mtendaji wa kituo hicho, Ephraim Mafuru, amewaeleza wahariri walioshiriki semina hiyo kwamba, kwa ushirikiano walionao, watahakikisha wanafikisha malengo waliyojiweka kwa mwaka 2023/2024, ya kukusanya shilingi bilioni 120, kwa mwaka.


Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa (AICC), Ephraim Mafuru

Mafuru amesema ambaye aliwaeleza wahariri na waandishi wa habari 
majukumu ya taasisi hiyo na  kuweka wazi lengo lao la kushiriki kuchangia pato la taifa na uchumi.


Amesema kiasi hicho cha fedha wanachotarajia kukusanya kwa mwaka, kitatoka AICC, JNICC, Hopitali ya AICC, ofisi na nyumba za makazi walizopangisha watu.


“Tumejipanga kukusanya zaidi ya shilingi bilioni 120, kupitia mikutano 30 kwenye kumbi zetu za AICC na JNICC, hospitali yetu na nyumba, tunaamini tutafanikiwa ukizingatia Rais Samia Suluhu Hassan, amekuwa kiongozi wa kutangaza fursa za mikutano hapa nchini," amesema.


Mkurugenzi huyo amesema kwa mwaka wa 2022/2023 waliandaa mikutano 18,  kwa mipango waliyojiwekea watahakikisha Tanzania inaongoza katika Bara la Afrika kuandaa mikutano mingi.


Amesema kwa mwaka wa fedha wa 2023/2024, wameandaa mikutano minne ya kimataifa ambayo ni  wa Rasilimali Watu, Jukwaa la Mifumo ya Chakula Afrika (AFS-Forum), ICMDA na PCCB, huku wakiwa na maombi mengi yanayoweza kufikisha lengo lao la mikutano 30.


Mkurugenzi Mtendaji huyo amesema  miaka ijayo wanatarajia kuandaa mikutano 50, itakayowezesha kuchangia zaidi ya shilingi bilioni 350, kwa mwaka, zikiwemo dola za Marekani.


Amesema AICC imechangia zaidi ya shilingi bilioni 5.4, JINCC shilingi bilioni 4.4, hospitali 
shilingi bilioni 4.5, huku wakiamini  zitapanda, huku akikiri kwamba, miaka ya nyuma walijiendesha kwa hasara.


Mafuru amesema kuanzia mwaka 2021/2022, wamejiendesha kwa faida, ambapo mwaka 2022 walipata faida ya shilingi bilioni 1.1, tofauti ya hasara ya shilingi milioni 500,  waliyopata miaka ya nyuma.



Mkurugenzi huyo amesema ili kufikia malengo waliyojiwekea hatamvumilia mtumishi atakayekwenda kinyume na makubaliano.


Madeni


Mkurugenzi huyo amesema mashirika  ya serikali zaidi ya 17,  yanaongoza kwenye orodha ya wadaiwa sugu wa vituo vya AICC na JNICC, ambapo taasisi za serikali zinadaiwa zaidi ya sh. bilioni 7.4.

 


Amesema pamoja na taasisi za serikali, pia wana tatizo kubwa la watu kulipa madeni, kwani hadi sasa wanadai zaidi ya bilion 7.4, huku taasisi za Serikali zikiongoza katika orodha hiyo ya wadaiwa sugu.


"Tuna shida kubwa ya watu kulipa madeni, hadi tunaandaa ripoti hii, AICC na JICC ilikuwa inadai taasisi zote na wateja shilingi bilion 7.4,  kati yao wadau wenye madeni makubwa ni taasisi za serikali.

 

"Ni ngumu kwa Mkurugenzi Mkuu kwenda kumdai Katibu Mkuu, ingawa kwenye mashirika binafsi tunawazuia, kama hawajalipa hawaingii hapa, lakini kuna njia ambazo tunatumia, tumeishirikisha bodi yetu na Katibu Mkuu na hapa Waziri ameshatoa taarifa hizi, taasisi zinazodaiwa zilipe madeni.



No comments