Header Ads

ad

Breaking News

Kombe la Diwani Kata ya Soga laanza kupigwa

                                                                          Kigero FC

Na Omary Mngindo, Kibaha

TIMU 10 za soka za vijiji vinavyounda Kata ya Soga Wilaya ya Kibaha Mkoa wa Pwani, zinashiriki Kombe la Diwani linaloratibiwa na Diwani,Shomali Minshee.


Timu hizo ni Vikuge Ray, Kigero FC, Coca Cola United, Misufini SC, Dragon FC, Soga Ranger's, Benabeu FC, Black Fighter, Sagare United na Msese FC.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi, Diwani wa kata hiyo, Shomali Minshehe, amesema kinyang'anyiro hicho kinachotimua vumbi kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Vikuge, kutakuwa na zawadi mbalimbali kwa washindi.

Alisema kuwa lengo la mashindano hayo ni kuibua na kuendeleza vipaji kwa vijana ili waweze kuonekana, hatimae wenye uwezo wachukuliwe na vilabu mbalimbali hapa nchini.

"Bingwa na mshindi wa pili watajinyakulia jezi, mshindi wa tatu ataondoka na mpira mmoja, mashindano yetu itafikia tamati Oktoba Mosi mwaka huu, mbali ya burudani pia itawapatia fursa vijana kuonesha vipaji vyao," amesema Minshehe.

Aliongeza kuwa, katika michezo hiyo kumekuwepo na ushindani mkubwa, huku akiwaomba wana Soga kuendelea kujitokeza kwa wingi kushuhudia kitimtim hicho kinacholenga kuibua na kuendeleza vipaji kwa vijana.

"Naungana na mwanamichezo namba moja Rais Samia Suluhu Hassan, katika kuunga mkono juhudi zake za kuunga mkono michezo, tunamshuhudia akizisaidia timu mbalimbali ili zifanye vizuri," amesema Minshehe.

 Ameongeza kwamba, "Tunashuhudia wachezaji wanavyofanya vizuri katika ligi zetu, wakiwemo wanaocheza nchi mbalimbali, wote wametokea pembeni mwa miji, nami nataka Soga itoe vijana watakaocheza ligi mbalimbali ndani na nje ya nchi," amesema Minshehe.


                                                                           Sagare United 

No comments