Header Ads

ad

Breaking News

Kamilisha ukarabati Uwanja wa Benjamin Mkapa kabla ya Oktoba 15- Dkt.Ndumbaro


 

Na Mwandishi Wetu

WAZIRI wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Damas Ndumbaro amemuagiza Mkandarasi anayekarabati Uwanja wa Benjamin Mkapa, Kampuni ya Beijing Construction Engineering Group (BCEG), kufanya kazi hiyo, kwa saa 24  siku zote za wiki ili kazi hiyo ikamilike kabla ya Oktoba 15, 2023.

Dkt. Ndumbaro alikutana na baadhi ya wataalam kutoka African Football League ambao wamewasili nchini kwa ajili ya ukarabati katika maeneo ambayo watafanya kwa gharama zao.

Waziri Ndfumbaro amekagua ukarabati wa uwanja huo pamoja na mradi wa ujenzi wa viwanja vya michezo na kupumzikia vinavyojengwa katika eneo changamani la michezo la jijini hapo.

No comments