Header Ads

ad

Breaking News

JKCI kutibu moyo kwenye maonesho ya Madini Mkoani Geita

Daktari bingwa wa magonjwa ya moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Salehe Mwinchete akimpima jinsi moyo unavyofanya kazi (Echocardiograph – ECHO) mkazi wa Geita wakati wa maonesho ya sita ya kimataifa ya Teknolojia ya Madini yanayofanyika katika Viwanja vya EPZA Bombambili mkoani Geita. JKCI inatoa huduma za uchunguzi na matibabu ya magonjwa ya moyo, Sukari kwenye damu na shinikizo la damu katika maonesho hayo.

Wananchi wa Mkoa wa Geita na mikoa ya jirani wakiendelea kupata huduma katika banda la Ta asisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakati wa maonesho ya sita ya kimataifa ya Teknolojia ya Madini yanayofanyika katika Viwanja vya EPZA Bombambili mkoani Geita. JKCI inatoa huduma za uchunguzi namatibabu ya magonjwa ya moyo, Sukari kwenye damu na shinikizo la damu katika maonesho hayo. Picha zote na JKCI

No comments