Header Ads

ad

Breaking News

EWURA YAFUNGIA VITUO VINGINE VYA MAFUTA

Meneja wa Mawasiliano na Uhusiano EWURA, Titus Kaguo 

Na Mwandishi Wetu

EWURA imevifungia vituo vingine viwili vya mafuta kwa kosa la kuhodhi mafuta, kati ya mwezi Julai na Agosti 2023, Vituo hivyo ni Rashal Petroleum Ltd-Mlimba, Mkoa wa Morogoro na Kimashuku Investment Co. Ltd-Babati, Mkoa wa Manyara.

Akizungumza na waandishi wa abari leo  Septemba 30,2023, Meneja wa Mawasiliano na Uhusiano EWURA, Titus Kaguo amesema wanapokifungia kituo kwa miezi sita, wanataka umma ufahamu, kwa sababu hawa ndiyo wanaochangia kusuasua kwa usambazaji wa mafuta hapa nchini.

Kaguo alisema pamoja na mafuta kuwepo nchini, changamoto ya upungufu wa mafuta katika maeneo mbalimbali ilichangiwa na baadhi ya wamiliki wa vituo kuhodhi mafuta ili kujipatia maslahi ya kibiashara, ikiwemo faida kubwa kutokana na ongezeko la bei za mafuta kinyume na sheria.

EWURA imetoa onyo kali kwa wauzaji wa Jumla na wamiliki wa vituo vya mafuta kuwa, Serikali inafuatilia suala hilo kwa karibu kupitia vyombo vyake mbalimbali na ikithibitika uvunjaji  wa sheria na kanuni umetendeka, hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao ikiwemo kuwafutia leseni zao za biashara.

Waandishi wa habari wakimsikiliza, Meneja wa Mawasiliano na Uhusiano EWURA, Titus Kaguo (hayupo pichani)

No comments