Diwani Kwaga aandaa Super Cup Kiwangwa
Diwani Malota Kwaga akikagua moja ya timu zinazoshiriki mashindano ya Kiwangwa Super Cup
Na Omary Mngindo, Kiwangwa
DIWANI wa Kata ya Kiwangwa katika Halmashauri ya Chalinze wilayani Bagamoyo Mkoa wa Pwani, Malota Kwaga, ameandaa michuano ya soka inayochezwa kwenye Uwanja wa Shule ya Sekondari Masugulu.
Jumla ya timu 13, za ndani ya kata hiyo na mbili kutoka kata ya jirani ya Msata, zitawania ubingwa wa michuano hiyo.
Mratibu wa mashindano hayo, Abubakari Juma,s ameema kuwa, kinyang'anyiro hicho kinapigwa kwenye viwanja vya Shule ya Sekondari,na Msingi Masugulu.
"Katika ufunguzi wa ligi yetu ilizikutanisha timu za Best Kid kutoka Msata iliyocheza na Kiwangwa Kids, ambapo Kiwangwa iliibuka na ushindi wa bao 1-0, lililowekwa wavuni na Tariki Makelele," amesema Juma.
Ameongeza kwamba, mchezo wa pili ulizikutanisha timu za Mwetemo dhidi ya Misani uliomalizika kwa sare ya mabao 3-3, mchezo ulioipigwa Uwanja wa Sekondari, mabao ya Mwetemo yalifungwa na Sabati mabao mawili na Kiputo bao, huku ya Misani yakiwekwa wavuni na Indinde mabao mawili na Shafii bao moja.
Mratibu huyo amesema mashindano hayo yaliyoanzishwa na Diwani Malota yanalenga kuwapatia burudani wana Kiwangwa na kuibua na kuendeleza vipaji kwa vijana kwa maslahi yao binafsi na taifa.
Akizungumzia zawadi kwa washindi, Mratibu huyo amesema, "Mshindi wa kwanza atapata ng'ombe, wa pili mbuzi na mfungaji bora naye atazawadiwa, hadi sasa anayeongoza kwa ufungaji ni mshambuliaji kutoka timu ya Mwetemo," amesema.
No comments